HOTUBA
YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA
KATIBA,
MHE. JOSEPH S. WARIOBA WAKATI WA KUKABIDHI
RIPOTI
YA TUME KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA,
MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE NA
RAIS WA
ZANZIBAR MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN;
TAREHE
30 DESEMBA, 2013, DAR ES SALAAM
________________
Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania;
Mheshimiwa
Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa
Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu;
Mheshimiwa
Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa
Rais wa
Zanzibar;
Mheshimiwa
Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar;
Mheshimiwa
Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania;
Mheshimiwa
Pandu
Ameir
Kificho,
Spika
wa
Baraza
la
Wawakilishi;
Mheshimiwa
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania;
Mheshimiwa
Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Mheshimiwa
Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Pili wa Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania;
1
Mheshimiwa
Mzee Benjamin Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania;
Waheshimiwa
Viongozi wote mliopo hapa;
Waheshimiwa
Mabalozi;
Ndugu
wananchi;
Mheshimiwa
Rais,
Kwa
makubaliano na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, tarehe 6 Aprili,
2012
ulituteua kuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
ulituapisha
tarehe 13 Aprili na tulianza kazi tarehe 2 mei, 2012. Tulikuwa
34,
yaani wajumbe 32 na Katibu na Naibu Katibu. Leo tuko hapa 32.
Kama
inavyofahamika tulimpoteza mjumbe mmoja, Dr. Sengondo Mvungi
katika
mazingira ya kusikitisha.Mungu aiweke roho yake mahali pema
peponi.
Mjumbe mwingine, ndugu John Nkolo, hayuko hapa kutokana na
matatizo
ya kiafya.
Hali yake inaendelea vizuri.
Vile vile mjumbe wa
sekretariati
ndugu Onorius Njole aliugua wakati Tume ilipokuwa
inasimamia
Mabaraza ya Katiba. Naye pia hali yake inaendelea vizuri.
Mheshimiwa
Rais,
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa miezi kumi na nane kwa Tume
kukamilisha
kazi yake.
Sheria pia ilitoa nafasi ya Tume kuongezewa
muda
usiozidi miezi miwili na Tume iliomba muda huo na ulitukubalia.
2
Kazi
tuliyopewa tumeikamilisha na leo tupo tayari kukabidhi kwako
na kwa
Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Ripoti yetu kama sheria
inavyoelekeza.
zifuatazo:-
Ripoti tunayoikabidhi inaambatana na taarifa saba
(i)
(ii)
Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
Maoni ya Mabaraza ya Katiba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri
ya
Muungano wa Tanzania;
(iii)
Maoni ya Wananchi kuhusu Sera, Sheria na Utekelezaji;
(iv)
Takwimu za Ukusanyaji wa maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko
ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(v)
Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania;
(vi)
Viambatisho vya Ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba; na
(vii)
Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa
Rais,
Kabla ya
kukabidhi Ripoti yetu naomba univumilie niweze kusema
machache
lakini kwa maneno mengi. Napenda kuanza na shukrani. Baada
ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukamilisha kazi hii,
shukrani
zetu kwanza ni kwako Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais wa
3
Zanzibar.
mliotupa.
Tunawashukuru kwa kututeua na pia kwa msaada mkubwa
Kila
tulipokwama mahali mlikuwa wepesi kutoa maagizo
yaliyotukwamua.
Tunawashukuru sana Mawaziri wa Katiba na Sheria,
Wanasheria
Wakuu wa Serikali, Makatibu Wakuu Viongozi na Watendaji
Wakuu wa
Wizara za Katiba na Sheria, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa
Wilaya,
Wakurungenzi na Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Watendaji
wa Tarafa, Kata na Shehia, Vijiji na Wenyeviti wa Serikali za
vijiji
kwa ushirikiano mzuri walioutoa kwa Tume.
Aidha, Tume inatoa
shukrani
za dhati kwa Jeshi la Polisi na Kamati za Ulinzi na Usalama za
Wilaya
kwa kuhakikisha mchakato mzima unakamilika kwa usalama.
Tume pia
inatoa shukrani kwa Vyama vya siasa, Jumuiya za Dini,
Asasi za
Kiraia, Taasisi na makundi mengine kwa mchango wao. Kwa
namna ya
pekee, tunavishukuru vyombo vya habari ambavyo, licha ya
kusambaza
taarifa
mbalimbali
zilizokuwa
zikitolewa
na
Tume,
vimeuelimisha
Umma na kuufanya mchakato mzima wa katiba kuwa wa
wazi na
wenye hamasa.
Mwisho
kwa uzito wa pekee Tume inawashukuru wananchi, hasa
wananchi
wa kawaida, kwa mchango wao mkubwa wa mawazo na maoni.
Hii ni
mara ya kwanza katika nchi yetu kwa wananchi wa kawaida
kushiriki
katika kutoa maoni kuhusu aina ya Katiba wanayoitaka na
wamefanya
hivyo kwa wingi na kwa uzito mkubwa.
4
Mheshimiwa
Rais,
Kama nilivyosema
mapema, pamoja na Ripoti ya Tume kuhusu
mchakato
wa katiba ambayo tunakabidhi leo, tunakabidhi pia na Rasimu
ya
Katiba. Rasimu hiyo ni ndefu kuliko Rasimu ya awali. Rasimu ya awali
ilikuwa
na ibara 240. Rasimu ya sasa ina ibara 271. Ongezeko la ibara
kwa
kiwango kikubwa limetokana na Tume kuzingatia maoni ya Mabaraza
ya
Katiba. Muhtasari wa Rasimu uko kwenye Sura ya Kumi na Mbili ya
Ripoti
yetu. Kwa leo nitagusia mambo machache ambayo Tume imeona
vyema
tukatoa maelezo.
Jambo la
kwanza, ni ushiriki wa wananchi katika mchakato mzima
wa
kupata katiba mpya. Tume ilipoanza kulikuwa na wasiwasi kwamba
ushiriki
wa wananchi wa kawaida ungekuwa dhaifu kwa sababu iliaminika
kwamba
wananchi kwa ujumla wao hawana ujuzi wa katiba. Lakini Tume
iligundua
mapema kwamba wananchi wanajua mambo mengi ambayo ni
msingi
wa katiba yoyote ile.
Sura
tano za mwanzo za Rasimu ya Katiba zinatokana na mchango
mkubwa
kutoka kwa wananchi, hasa kuhusu Misingi ya Taifa, Tunu za
Taifa,
Maadili na Miiko ya Uongozi, Dira ya Taifa na Haki za binaadam.
Wananchi
pia wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala wa
nchi,
ikiwa ni pamoja na nafasi ya wawakilishi wao Bungeni.
5
Hii ni
mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwashirikisha kwa ukamilifu
wananchi
katika kutunga katiba ya nchi yao. Nia ya mchakato huu ni
kupata
katiba inayokubalika na wananchi. Ili katiba ikubalike na wananchi
ni jambo
la msingi maoni yao yapewe uzito unaostahili. Nayasema haya
kwa
sababu tangu Rasimu ya kwanza itolewe maeneo yaliyopewa uzito
na
wananchi hayakupewa uzito katika mijadala ya viongozi, wasomi na
vyombo
vya habari.
Mheshimiwa
Rais,
Utangulizi
wa Katiba unaeleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania imetungwa na Wananchi wa Tanzania. Utangulizi
unatoa
taswira na picha halisi ya Jamhuri ya Muungano na watu wake,
historia
yao, matarajio yao, misingi ya taifa na masuala muhimu ambayo
Wananchi
wanataka kuyaendeleza katika jamii, kizazi hadi kizazi.
Sura ya
Kwanza inaelekeza kuendelea kuwepo kwa Jamhuri ya
Muungano
wa Tanzania. Yapo pia masharti kuhusu alama za Taifa na
sikukuu
za Taifa na Rasimu inatambua Lugha ya Kiswahili kuwa Lugha ya
Taifa.
Imeainisha pia tunu za Taifa ambazo ni Uhuru, Haki, Udugu,
Amani,
Usawa, Umoja na Mshikamano. Tunu za Taifa ndiyo msingi wa
maadili
na taratibu mbalimbali za kimaisha za jamii mbali mbali ambazo
hurithishwa
kizazi hadi kizazi.
6
Mheshimiwa
Rais,
Dira ya
Taifa ni eneo ambalo wananchi walilitolea maoni kwa wingi
na kwa
uzito. Sura ya Pili ya rasimu kuhusu malengo muhimu, misingi ya
mwelekeo
wa shughuli za Serikali na sera za kitaifa imejumuisha maoni
mengi ya
wananchi. Wakulima, wafugaji, wavuvi na makundi mengine
wanataka
kuwe na dira ya Taifa ambayo ndiyo itakuwa mwongozo mkuu
utakaofuatwa
na kuzingatiwa na uongozi, hasa Serikali na vyama vya
siasa
katika kutekeleza shughuli za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni
na
kimazingira.
Sura ya
Tatu imependekeza masharti kuhusu Maadili na Miiko ya
Uongozi
na Utumishi wa Umma. Uongozi ni dhamana, na kiongozi wa
Umma
anatakiwa kutekeleza wajibu wake kwa kuheshimu Wananchi,
kukuza
hadhi ya Taifa na kukuza imani na heshima ya Utumishi wa Umma
kwa Wananchi.
Rasimu imeorodhesha miiko ya uongozi ikiwa ni pamoja
na
kupiga marufuku kiongozi wa Umma kutumia wadhifa, nafasi ya
madaraka
au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu,
jamaa,
marafiki au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu.
Mheshimiwa
Rais,
Sura ya
Nne, inahusu Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia na
Mamlaka
za Nchi.
Wananchi wametoa maoni mengi kuhusu haki za
7
binadamu
na hasa katika suala la utekelezaji na usimamizi wa haki hizo.
Kutokana
na maoni ya Wananchi, Rasimu imeboresha haki za binadamu
zilizomo
katika Katiba ya sasa na kuongeza haki mpya za mtu binafsi na
haki za
makundi mbalimbali kama vile watoto, wanawake, wazee, vijana,
makundi
madogo katika jamii, watu wenye ulemavu, wafanyakazi, waajiri
na haki
ya kutafuta, kutoa na kusambaza habari.
Aidha, Rasimu
imeainisha
wajibu wa raia ikiwa ni pamoja na kulinda na kutetea Katiba
na
Sheria za Nchi; kulipa kodi, kuheshimu haki, uhuru na maslahi ya watu
wengine
na kulinda na kutunza mazingira.
Sura ya
Tano inahusu Uraia wa Jamhuri ya Muungano. Uraia ni
mmoja,
nao ni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rasimu ya Katiba
inapendekeza
kutambuliwa kwa uraia wa kuzaliwa na kujiandikisha
ambao ni
wa nchi moja.
Aidha, Rasimu inapendekeza kuwapa hadhi
maalum
watu wenye asili au nasaba ya Tanzania ambao wameacha kuwa
raia wa
Tanzania kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine.
Mheshimiwa
Rais,
Kuhusu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Rasimu ya Katiba
imefafanua
kwa kina na ufasaha juu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
ambaye
ni alama na taswira ya nchi na Watu wake. Yeye peke yake
ndiye
mwenye hadhi na heshima ya Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na
8
Kiongozi
wa Serikali. Kwa kuzingatia maoni ya Wananchi, madaraka ya
Rais na
hasa yale ya uteuzi yamepunguzwa kwa kuweka vyombo vya
kupendekeza
majina ya Watu wa kuteuliwa na kwa baadhi ya vyeo
kuhitaji
kuthibitishwa na Bunge.
Mheshimiwa
Rais,
Wananchi
wametaka Katiba itambue mamlaka na madaraka
yao
juu ya
wawakilishi wao katika Bunge, na kama ilivyokuwa katika Rasimu
ya
Awali, inapendekezwa Wabunge wasiwe Mawaziri, kuwe na ukomo wa
uwakilishi
katika Bunge na wapiga kura wawe na madaraka ya
kumwajibisha
Mbunge hata kabla ya kumalizika kwa muhula wake na
Spika na
Naibu Spika wasitokane na Wabunge au kiongozi wa juu wa
chama
cha siasa.
Kuhusu
Mahakama ya Jamhuri ya Muungano, Sura ya Kumi imebaki
na
mapendekezo ya awali ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu
(Supreme
Court) na kuendelea kuwepo kwa Mahakama ya Rufani. Aidha,
inapendekezwa,
kama ilivyo katika Katiba ya sasa, Mahakama Kuu ya
Tanzania
Bara (Tanganyika) na Mahakama Kuu ya Zanzibar, ziendelee
kuwa na
mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali, mashauri ya
madai na
jinai yanayohusu sheria za Serikali ya Jamhuri ya Muungano
katika
maeneo yao ya utawala (concurrent jurisdiction).
9
Mheshimiwa
Rais,
Tume kwa
kuzingatia maoni ya Wananchi, tofauti na ilivyokuwa
katika
Rasimu ya Awali, sasa inapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa
iwe ni
taasisi inayojitegemea na siyo kuwa Sehemu ya Tume Huru ya
Uchaguzi.
Kuhusu
ulinzi na usalama, Sura ya Kumi na Tano inatamka kuwa
jukumu
la ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano ni la kila raia.
Kwa
kuzingatia maoni ya Wananchi waliyoyatoa katika Mabaraza ya
Katiba,
Rasimu sasa inapendekeza kuwepo kwa Jeshi la Polisi moja na
Idara ya
Usalama wa Taifa moja katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mheshimiwa
Rais,
Mabadiliko
makubwa ya Katiba lazima yaendane na masharti
yatokanayo
na Masharti ya Mpito ambayo nayo ni sehemu ya Katiba.
Masharti
haya yanaweka utaratibu, mfumo wa kikatiba na kisheria kuhusu
masuala
ya kiutawala, uongozi wa nchi, sheria za nchi, nafasi za
madaraka
na namna mambo yote hayo yatakaavyokuwa na kuendeshwa.
Sura ya
Kumi na Saba inapendekeza Muda wa Mpito wa Miaka
Minne,
kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba Mpya hadi tarehe
31
Desemba, 2018.
Katika kipindi hicho, sheria zilizopo hivi sasa
10
zitaendelea
kutumika hadi zitakapobadilishwa.
Sheria zinazotumika
Tanzania
Bara zitakuwa za Tanganyika na sheria zinzotumika Tanzania
Bara na
Zanzibar zitakuwa Sheria za Jamhuri ya Muungano. Yapo pia
mapendekezo
kuhusu masuala ya kufanyiwa kazi katika Muda wa Mpito.
Mambo
haya ni pamoja na:-
(i)
(ii)
(iii)
(iv)
(v)
(vi)
Kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika;
Kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 ili kuwiana
na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 2014;
Mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali za Nchi washirika;
Kuundwa kwa Tume na Taasisi za Kikatiba zilizoainishwa
kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Mwaka 2014 na kwa kuzingatia masharti ya Katiba hiyo;
Kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano ya Mwaka 2014; na
Kufanya maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajili ya
utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka
2014.
11
Mheshimiwa
Rais,
Moja ya
mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu
Rasimu
ya awali ilipotolewa na Tume ni Muungano wa Tanzania.
Jambo
kubwa
limekuwa juu ya muundo wa Muungano. Wakati Tume inazindua
Rasimu
ya Awali tulisema hatukupendekeza kuendelea kuwa na muundo
wa
Serikali mbili kwa sababu mbalimbali. Tulisema kuwa kuendelea kwa
Serikali
mbili kulihitaji ukarabati mkubwa ambao tulifikiri hautawezekana.
Mabaraza
ya Katiba yalitoa maoni mengi ambayo yaliilazimu Tume
kufanya
tena uchambuzi wa kina.
Kama ilivyokuwa katika Rasimu ya
Awali,
suala la muundo wa Muungano ndilo lililochukuwa muda mwingi
wa Tume.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilielekeza kwamba Tume
itaongozwa
na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na
kudumisha
mambo kadhaa. Moja ya mambo hayo ilikuwa ni kuwepo kwa
Jamhuri
ya Muungano.
Hivyo, Tume ilianza kazi kwa madhumuni ya
kupata
maoni ya kuboresha Muungano. Wananchi wengi walitoa maoni
kuhusu
Muungano, lakini wengi wao walijikita kwenye Muundo wake.
Kwa
Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu
Muungano
na kati ya hao, karibu 27,000 walizungumzia muundo. Kwa
Zanzibar,
wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwenye suala la
Muungano.
Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni Wananchi
19,000
walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano.
12
Mchanganuo
wa takwimu hizi unaonyesha kuwa kwa upande wa
Tanzania
Bara, 13% walipendelea Serikali moja, 24% walipendekeza
Serikali
mbili na 61% walipendekeza Serikali tatu.
Kwa upande wa
Zanzibar,
34% walipendekeza Serikali mbili na 60% walipendekeza
Muungano
wa Mkataba, na 0.1% (watu 25) walipendekeza Serikali moja.
Aidha,
taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na jumuia
za
kidini zilipendekeza muundo wa Serikali tatu.
Baadhi ya taasisi za
kiserikali,
ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya mapendekezo yao, pia
zilipendekeza
Serikali tatu. Kwa mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar
lilipendekeza
kuwepo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya
Tanganyika
na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi maeneo, uwezo,
nguvu,
utendaji na mipaka ya kila mamlaka.
Ofisi ya Waziri Mkuu
imependekeza
mfumo wa serikali tatu ili kuondoa kero za muungano.
Aidha,
Mamlaka ya Mapato Tanzania imependekeza kuwepo kwa Serikali
tatu ili
kutoa majibu ya kero zilizopo na kuleta utulivu zaidi ilimradi
upangiliwe
vizuri.
Mheshimiwa
Rais;
Baada ya
kuona takwimu hizi na kuchanganua sababu zilizotolewa
na
makundi mbali mbali, Tume iliamua kufanya utafiti kuhusu muundo wa
Muungano.
Suala hili lilijitokeza kwa nguvu na hisia kali mara ya kwanza
mwaka
1984 katika kipindi kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa
13
kisiasa
Zanzibar”. Mwaka 1991 Tume ya Nyalali ilipendekeza Muundo wa
Serikali
tatu.
Miaka miwili baadaye, yaani Mwaka 1993, kikundi cha
Wabunge
wa
Tanzania
Bara
katika
Bunge
la
Muungano,
G55,
kilipendekeza
kuwa na muundo wa Serikali tatu na Bunge likaridhia.
Mwaka
1999 Kamati ya Kisanga ilipendekeza muundo wa Serikali tatu.
Tume pia
imepitia taarifa ya Kamati nyingi zilizoundwa na Serikali ya
Jamhuri
ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama vile,
Kamati
ya Amina Salum Ali na Kamati ya Shelukindo ya mwaka 1994.
Sababu
zilizotolewa katika matukio hayo ya mwanzo kwa kiwango
kikubwa,
zinafanana na zile ambazo zimetolewa kipindi hiki. Kila upande
wa
Muungano una malalamiko mengi kuhusu muundo wa Muungano.
Katika
Taarifa ya Tume tunayokukabidhi leo, tumeorodhesha malalamiko
kumi kwa
upande wa Zanzibar na malalamiko manane kwa upande wa
Tanzania
Bara. Kwa upande wa Zanzibar malalamiko matatu makubwa
ni;
(i)
(ii)
Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Serikali ya Muungano
ambalo linaisaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Koti hilo
limeifanya Tanganyika kuwa ndiyo Tanzania;
Mambo ya Muungano yamekuwa yakiongezeka na hivyo
kuathiri madaraka ya Zanzibar (autonomy) na kufifisha hadhi
ya Zanzibar (identity) na Zanzibar inaendelea kumezwa; na
14
(iii)
Kumwondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri
ya Muungano.
Kwa
upande wa Tanzania Bara, malalamiko makubwa ni;
(i)
Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo
wake wa Taifa ina Serikali yake na imebadili Katiba yake ili
ijitambue kama nchi, wakati Tanzania Bara imepoteza
utambulisho
wake.
Katiba ya Jamhuri inasema Tanzania ni
nchi
moja lakini Katiba ya Zanzibar inasema ni nchi mbili;
(ii)
(iii)
Zanzibar imebadili Katiba yake na kuchukua madaraka ya
Jamhuri ya Muungano, kama vile kuelekeza sheria za
Muungano zilizopitishwa na Bunge la Muungano zipelekwe
kwenye Baraza la Wawakilishi. Maana yake ni kuwa Katiba ya
Zanzibar sasa ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano; na
Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki
ardhi
Zanzibar wakati wenzao wa Zanzibar wana haki hiyo
Tanzania
Bara.
Mheshimiwa
Rais;
Katika
kuchambua malalamiko ya Zanzibar kwamba Tanganyika
imevaa
koti la Muungano, Tume imebaini kwamba muundo wa Muungano
wa Serikali
mbili umeifanya Serikali ya Muungano kwa kiwango kikubwa
15
kushughulikia
zaidi mambo ya Tanzania Bara, hasa mambo ya
maendeleo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka
1977,
Serikali ya Muungano ina mamlaka ya kusimamia mambo ya
muungano
na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania
Bara.
Kwa msingi huo, Serikali ya Muungano inashughulikia sana mambo
ya
kilimo, elimu, afya, maji, nishati na madini, ujenzi, uchukuzi, maliasili
na
utalii na mengine ya Tanzania Bara ambayo siyo mambo ya
Muungano.
Wakati wa kikao cha Bajeti Bunge la Muungano hutenga siku
mbili au
tatu za majadiliano kwa Wizara zinazosimamia mambo haya
yasiyo
ya Muungano ya Tanzania Bara wakati mambo ya Muungano kama
vile ulinzi,
mambo ya nje na mambo ya ndani hutengewa siku moja au
nusu
siku.
Maswali ya Wabunge kuhusu mambo ya maendeleo pia
yanahusu
Tanzania Bara na ziara za Wabunge kukagua miradi ya
maendeleo
zinahusu Tanzania Bara katika mambo yasiyo ya Muungano.
Mambo
haya Bungeni yanasimamiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano
ambaye, kihalisia hana mamlaka wala madaraka yoyote
kuhusu
Zanzibar.
Aidha,
muundo huu wa muungano pia umesababisha kuwepo kwa
wizara
au taasisi zenye sura au zinazotekeleza mambo ya muungano
pekee;
mambo ya Tanzania Bara na mambo mchanganyiko; kwa maana
ya mambo
ya muungano na mambo yasiyo ya muungano, hali ambayo
16
inapekea
ugumu wa kutofautisha gharama za muungano na zisizo za
muungano
katika wizara au taasisi hizo. Kundi la pili na la tatu ndio
imekuwa
chanzo cha kero za muungano.
Hakuna
njia ya kubadili hali hii kwa sababu Serikali ya Muungano
haina
mamlaka ya kutosha juu ya mambo ya maendeleo kwa upande wa
Zanzibar.
Mawaziri wengi na Serikali kwa ujumla inalazimika kupanga
maendeleo
na kutafuta rasilimali kwa ajili ya Tanzania Bara zaidi kuliko
kwa
Zanzibar. Zanzibar hufanya mipango yake ya maendeleo. Lakini, ili
kupata
rasilimali kama mikopo na misaada ni lazima ipitie Serikali ya
Muungano,
jambo ambalo utekelezaji wake umesababisha matatizo
mengi.
Utatuzi wa matatizo hayo umekuwa mgumu, umechukua muda
mrefu au
umeshindikana. Njia pekee ambayo ingefanya maendeleo ya
Zanzibar
yapewe uzito sawa na mambo ya Tanzania Bara ni kuyaweka
mambo
hayo chini ya Serikali ya Muungano, yaani kuwa na Serikali moja.
Hata
hivyo, hilo likifanyika kuna hofu ya Zanzibar kumezwa.
Mheshimiwa
Rais;
Tume imefanya
uchambuzi wa ndani kuhusu malalamiko ya
Zanzibar
kwamba kuongezeka kwa Mambo ya Muungano kumeathiri
madaraka
ya Zanzibar (autonomy). Tangu mwanzo wa Muungano,
ilikubalika
kwamba Zanzibar ibaki na hadhi yake na iwe na madaraka
17
kuhusu
Mambo yasiyo ya Muungano. Tume ilifanya uchambuzi wa Mambo
ya
Muungano ili kubaini kama yanaingilia hadhi na uhuru wa Zanzibar.
Kati ya
Mambo 22 ya Muungano, Tume imebaini kuwa siyo mambo yote
yanatekelezwa
kikamilifu kimuungano. Mambo mengi yamebadilishwa bila
ya
kubadili katiba, ama kwa makubaliano kati ya pande zote mbili za
Muungano
au kwa hatua zilizochukuliwa na upande mmoja. Mambo hayo
ni
pamoja na kodi, bandari, leseni za viwanda, usafiri na usafirishaji wa
anga,
utafiti, posta na simu, uraia, takwimu, mafuta na gesi na
Mahakama
ya Rufani.
Kwa hali
halisi ilionekana hakuna uwezekano kuyarudisha kwenye
orodha
ya muungano mambo ambayo yameondolewa kiutekelezaji.
Kwa
kipindi cha miaka ishirini iliyopita, Kamati nyingi zimeundwa na
kutoa
mapendekezo ya kuondoa mambo mengi zaidi kutoka kwenye
Orodha
ya Mambo ya Muungano, ikiwa ni pamoja na elimu ya juu,
biashara
ya nje, uhusiano wa kimataifa, mikopo, misaada ya nje na
mafuta
na gesi. Wakati Tume inakusanya maoni, Wananchi wengi wa
Zanzibar
kutoka makundi mawili makubwa, yaani wale waliotaka
Muungano
wa Serikali Mbili na wale waliotaka Muungano wa mkataba,
wote
walipendekeza mambo hayo yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo
ya
Muungano.
18
Kwa
tathmini ya Tume baadhi ya mambo haya hakuna budi
yaondolewe
kutoka orodha ya muungano la sivyo kero za muungano
zitaendelea.
Kwa mfano suala la uhusiano wa kimataifa likiendelea kuwa
ni jambo
la muungano Zanzibar haitaweza kujiunga na mashirika kama
OIC na
FIFA. Kwa msingi huo, Tume imependekeza kuliondoa suala la
uhusiano
wa kimataifa katika mambo ya muungano na kubakisha suala la
mambo ya
nje.
Eneo
jingine ni mgongano kati ya Katiba ya Muungano, na Katiba ya
Zanzibar.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeweka masharti kwamba
sheria
zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano hazitatumika
Zanzibar
hadi zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi. Aidha, kodi
itakayoamuliwa
na Bunge kutozwa na Serikali ya Muungano lazima ipate
ridhaa
ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mambo
haya yameleta mgongano wa Katiba. Juhudi zilizofanywa
na pande
zote mbili hazikufanikiwa kuondoa mgongano huo.
Zaidi ya
hapo, mabadiliko
ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanywa mwaka 2010
yametamka
wazi kwamba Zanzibar ni nchi kati ya nchi mbili za Muungano
wakati
Katiba ya Jamhuri inaelekeza kwamba
Tanzania ni Nchi moja.
Mabadiliko
katika Katiba ya Zanzibar pia yamehamisha baadhi ya
madaraka
ya Serikali ya Muungano kwenda Zanzibar.
19
Wakati
wa kukusanya maoni ya wananchi, Tume ilibaini kwamba
haitakuwa
rahisi kubadili Katiba ya Zanzibar kuifanya Zanzibar kuonekana
kuwa
sehemu ya Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa sura ya nchi
kamili.
Mabadiliko ya aina hiyo yatahitaji kura ya maoni kama Katiba ya
Zanzibar
inavyoelekeza. Kwa tathmini ya Tume, baada ya kuwasikiliza
wananchi
wa Zanzibar, ni dhahiri kwamba pendekezo la kuifanya Zanzibar
isionekane
kama nchi halitakubalika kwenye kura ya maoni.
Kwa
kifupi tathimini yetu ni kwamba ukarabati mkubwa unahitajika
ili
kuendelea na muundo wa Serikali mbili.
Maeneo mawili makubwa
yanahitaji
mabadiliko. Jambo la kwanza ni kuwa na mambo ya kutosha
kwenye
orodha ya muungano, ikiwa ni pamoja na mambo ya maendeleo
na
kiuchumi. Jambo hilo likifanyika, litazidisha malalamiko kwa upande
wa
Zanzibar kuwa hadhi na madaraka yake yanazidi kupotea. Aidha,
Mambo ya
muungano yakipunguzwa sana Serikali ya Muungano itakuwa
inashughulika
zaidi na zaidi na mambo ya Tanganyika; na Zanzibar itaona
Tanganyika
ndiyo muungano. Lakini kwa upande mwingine, Tanganyika
nayo
itaona si haki nayo isiwe na uhuru wa kuendesha mambo yake kama
ilivyo
kwa Zanzibar.
Jambo la
pili ni kuondoa mgongano na mgogoro wa Katiba. Hiyo
maana
yake ni Zanzibar kubadili Katiba yake ili Zanzibar na Tanganyika
ziwe ni
sehemu za nchi moja badala ya kuwa nchi kamili. Kama Zanzibar
20
na
Tanganyika zikiwa nchi kamili haitawezekana nchi moja ikawa na
hadhi na
uhuru wake na nchi nyingine isiwe na hadhi na uhuru
(autonomy)
wake.
Kwa
tathimini ya Tume, kwa hali halisi, tunaona ukarabati huo ni
mgumu.
Hii ndiyo sababu kubwa ya kupendekeza muundo wa Serikali
tatu ili
pande zote mbili ziwe na hadhi sawa. Kila upande utashughulikia
mambo
yasiyo ya muungano na Serikali ya Muungano itabaki na mambo
machache
ya msingi na ambayo yanaunganisha taifa.
Mheshimiwa
Rais;
Wakati
muundo wa Serikali tatu unaonekana kukidhi matakwa ya
watanzania
walio wengi na pia kushughulikia ipasavyo mengi ya matatizo
ama
malalamiko au kero za Muungano, Tume imetambua kuwa muundo
huo nao
una changamoto zake. Ili kujikinga na changamoto hizo Tume
imependekeza
mambo matatu.
Jambo la kwanza ni uraia.
Tume
imependekeza
uraia uwe mmoja na raia wote wa Jamhuri wawe huru na
wawe na
haki zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi nzima
isipokuwa
katika mazingira maalum.
Haki zao zikiingiliwa na upande
wowote
bila sababu maalum itapelekea kuibuka kwa utaifa; Utanganyika
au
Uzanzibari, na uzalendo utayumba. Uzalendo ukiyumba na muungano
pia
utayumba.
21
Pili ni
Serikali ya Muungano kuwa na uhakika wa mapato kwa ajili ya
kulipia
gharama za Muungano. Tume imependekeza ushuru wa bidhaa
uwe ni
kodi ya Muungano. Kodi hii itakidhi sehemu kubwa ya matumizi
ya
Muungano na sehemu itakayobaki itapatikana kutokana na mapato
yasiyo
ya kodi yanayotokana na mambo ya muungano, michango ya Nchi
Washirika
na mikopo.
Tatu ni kuundwa kwa Tume ya Uhusiano na
Uratibu
wa Serikali chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Muungano
na
itajumuisha viongozi wakuu wa nchi washirika. Majukumu ya Tume
hiyo ni
kusimamia mashauriano na mashirikiano kati ya Serikali ya
Muungano
na Serikali za nchi washirika ili kuhakikisha sera zinawiana na
pia
kusimamia na kuimarisha masuala yenye maslahi kwa taifa na pia
kutatua
migogoro.
Mheshimiwa
Rais;
Kazi hii
haikuwa rahisi hata kidogo.
Sisi wajumbe kila mmoja
tulikuwa
tumetoka kwenye makundi tofauti tofauti.
Kila mmoja wetu
alikuwa
na imani yake, maono yake, itikadi yake, msimamo wake na
kadhalika.
Lakini tulikubaliana mapema kabisa kwamba wajibu wetu ni
kwa
taifa.
Kwa hivyo, tuliacha imani na misimamo yetu binafsi na
kuamua
kuwasikiliza wananchi kwa makini sana.
Majadiliano yetu
yalilenga
kupata mwafaka wa kitaifa.
maridhiano.
22
Matokeo yake ni maamuzi ya
Baadhi
ya mapendekezo yetu kwa hakika yatapokelewa kwa
hamasa
kubwa. Lakini la muhimu ni kupata mwafaka wa kitaifa badala
ya
kufikia uamuzi kwa kujipima katika makundi.
Baada ya
kusema hayo machache lakini kwa maneno mengi, kwa
heshima
kubwa, naomba sasa kwa niaba ya Tume, kama sheria
inavyoelekeza,
nikukabidhi wewe Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais
wa
Zanzibar, Ripoti
ya Tume pamoja na Viambatanisho
vyake Saba,
ikiwemo
Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
23