Wahitimu watarajiwa wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) katika Kitivo
cha lugha za kigeni na isimu wametakiwa kujipamba kwa tabia njema ili
kukabiliana na changamoto za ajira baada ya kuhitimu kwao.
Aidha, wametakiwa kujenga utamaduni wakujiamini kutokana na kile
walichojifunza katika kipindi chote cha masomo chuoni hapo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Ofisi ya makamu Mkuu wa chuo
kikuu cha Dar es salaam, Dr Rose Upor wakati akitoa
nasaha zake za mwisho kwa wanafunzi hao katika mkutano maalumu uliofanyika
katika chumba cha SR15 chuoni hapo.
Drt Upor ambaye pia ni mlezi
wa wanafunzi hao hasa kupitia chama cha wanaisimu wa lugha za kigeni chuoni
hapo (DUFLLA) amesema, maisha ni safari ndefu ambayo inahitaji uvumilivu na
kamwe sio kupita katika njia za mkato kwani kufanya hivyo kunaweza
kuwahatarishia mustakbali wa maisha yao.
Aidha, amewaasa wanafunzi hao
kupanua maarifa yao katika kubuni njia mbalimbali zitakazowakwamua kimaisha
badala tu ya kutegemea kipato kupitia kuajiriwa.
Amewahakikishia wanakitivo
hicho kuwa, ni lazima wajiamini kuwa ni watu muhimu katika jamii na hasa
kutokana na uwezo wao wa kielimu na maarifa kiasi kwamba wanaweza kufanyakazi
katika sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Amesema, lazima kila mmoja
ajithamini yeye mwenyewe huku wakitambua kuwa hakuna kitu kisichowezekana
katika kupambana na maisha licha kwamba ni safari ndefu inayohitaji uvumilivu.
Kwa upande wake mwakilishi wa
wanafunzi hao ambae pia ni Raisi wa (DUFLLA) Mtoga Athumani, amemshukuru sana
Dkt Upor kwa kukubali mwaliko huo na kumtaka kuwa tayari kushirikiana nao kwa
hali na mali wakati wowote watakapo mhitaji.
Aidha ametumia fursa hiyo
kumhakikishia Dtr. Upor kuwa, akiwa kama Raisi wa chama hicho, atahakikisha (DUFLLA)
imesimama na kuendelea kuiunga mkono bega kwa bega wakiwa chuoni na hata nje ya
chuo hicho.
Mwisho Drt. Uppor
amewahakikishia wanafunzi hao kuwa yupo tayari kushirikian nao katika mazingira
yote watakayomuhitaji
Ikumbukwe kuwa Drt Uppor ni
mlezi wa Chama hicho na pia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha chama hicho
kinaelekea katika mafanikio.
No comments:
Post a Comment