Monday, June 2, 2014

SIKU YA KISIMAMO: USTADH MUBARAKA



UNIVERSITY OF DAR ES – SALAAM
DADILI ZA SIKU YA QIYAMA(SIKU YA KISIMAMO)
SIGNS OF THE DOOMSDAY




MUBARAKA    A    HAMAD.

فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّى لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ     [محمد : 18]
“Kwani wanangoja lingine ila kiama kiwajie? basi alama zake zimekwisha kuja, kutawafaa nini wakati kitakapowajia”  ( Muhammad : 18).

Siku ya Qiyama (doomsday) ni siku ya hukumu ambayo waja wote wa Allah (S. W), watasimamishwa katika uwanja wa hukumu mbele ya Mfalme Muadilifu Allah (S. W) ili kulipwa jaza ya amali zao walizoweza kuzichuma kipindi chote cha uhai wao huko duniani.
Kwa kila Muumini ni lazima kuwa na yakini juu ya siku hii isiyokua na shaka, ili kukamilisha nafasi ya imani yake.
Hata wataalamu wa sayansi leo hii wanathibitisha kua kuna mwisho wa ulimwengu(maisha), Suala limekua ni vipi maisha yatakwisha. Kama waislam hatuna chembe ya shaka juu ya suala la kiyama. Allah anasema;

قال تعالى : {فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّى لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ}     [محمد : 18]
 Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): {Kwani wanangoja lingine ila kiama kiwajie? basi alama zake zimekwisha kuja, kutawafaa nini wakati kitakapowajia} ( Muhammad : 18).

“Hudhaifa ibn Asiid radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: (Tulikuwa tumekaa katika kivuli cha chumba cha Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) tukataja kiama na sauti zetu zikawa juu (mpaka Mtume akasikia) akasema : Hakitasimama au hakitakuwa kiama mpaka kupatikane kabla yake alama kumi)”

Kuhusu lini kiyama kitasimama, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amebainisha ya kwamba siku ya kiama haijulikani ni wakati gani na wala hakuna anayejua isipokuwa yeye peke yake. Na hakumhusisha yoyote kukijuwa kiama si Malaika aliyekurubishwa wala Mtume aliyetumilizwa na Mwenyezi Mungu wala binadamu wa aina yeyote ile. Pia imebainishwa kwamba kiama kimekaribia wakati wake kama zilivyoeleza  Aya za Quran Tukufu na hadithi za Bwana Mtume (SAW).  Allah (S. W) anasema.

قال تعالى {يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ}  [الأعراف : 187].
 Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala): Amesema: {Wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu hakuna wa kudhihirisha wakati wake ila yeye. Imekuwa nzito mbingu na ardhi, hakita kujilieni (kiama) ila ghafla wanakuuliza kana kwamba unaelimu nacho, waambie (ewe Muhammad) hakika simengineyo ilimu yake ipo kwa kwa allah tu, lakini wengi katika watu hawafahamu.(Al-Araaf : 1870).

Pia Allah (S .W) akaendelea kuzidi kuweka msisitizo katika Suratul – Ahzab.  

وقال : {يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِنْدَ اللَّهِ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا}    [الأحزاب : 63]
Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala):  {Watu wanakuuliza kuhusu kiama kitakuja lini? sema: ilimu yake iko kwa Mola wangu tu. Na kipi kitakacho kujulisha lini kiama, pengine kiama kiko karibu} (Al-Ahzab : 63).

Kama hayo hayatoshi, Mtume (S.A. W) alibainisha wazi kuhusu suala la qiyama, pale alipoulizwa na Malaika Jibril kuhusu  Qiama
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akajibu:  (hakuwa mwenye kuulizwa ni mjuzi kuliko anayeuliza" 
  Kuhusu elimu ya Qiyama, Uhakika wake upo kwa Mola tu pekeyake, Sisi letu ni kutambua dalili au ishara za kukaribia kwake, nazo zipo wazi na ukweli kimesha karibia kama mwenyewe anavyo tubainishia.
قال تعالى : { وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا} [الأحزاب : 63]
    
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema: {Na kipi kitakujulisha lini kiama pengine kiko karibu (63) 
Chakusikitisha na kushangaza ni kwa huyu mwanadamu anayeonekana kuendelea kughafilishwa na haya maisha yenye kudanganya na yamuda mfupi. Allah (S. W) amesema.
قال تعالى : {اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُعْرِضُونَ} [الأنبياء :1]
Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: { imekaribia watu hisabu yao (ya kiama) nao wamo katika kughafilika na wanalipuuza}} [Al-Anbiya :1]. 
Katika kuonesha ukaribu wa Qiyama Mtume (S A W) anasema 
“Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili” Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada.

VIGAWANYO VYA DALILI ZA QIYAMMAH

DALILI KUBWA (MAJOR SIGNS). Hizi ni dalili za mwisho mwisho kabisa ambazo kutokea kwake zitakua zina fuatana hadi Qiyammah kisimame. Ni mambo yasiyo ya kawaida kama vile tutakavyo yaona.

DALILI NDOGONDOGO (MINOR SIGNS). Ni dalili au alama katika maisha ya kawaida zilizo bashiriwa na mtume Muhammad (SAW) kua zitatokea kabla ya Qiyama kusimama. Ni dalili za kuwazindua walioghafilika na Ghururi ya Ulimwengu, na matamanio yake. Ama kuhusu dalili hizi nyingi zimesha tokea na kuonekana, jambo lililowafanya Waislamu waongezeke imani na kumsadiki zaidi Mtume wao, miongoni mwa alama hizo ni pamoja na zifuatazo.

1) Ujiyo wa Mtume Muhammad {The comming of prophet Muhammad (SAW)
 Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: (Nimetumilizwa na kiama kama vidole viwili). Akashiria vidole viwili cha kati na cha shahada.
(a) Muhamad  (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kuletwa kama Mtume wa ulimwengu mzima
(b) Muhamad  (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) kukamilisha utumwa wa Allah (Subhanahu wa taala)

 2) Kufariki kwa  Mtume Muhammad The death of Prophet Muhammad (SAW)

3)  Kudhihiri fitna kubwa (Evidenced of great mischief); mpaka ikafikia hali ya kuchanganyika haki na batili mpaka mtu ataamka asubuhi hali ya kuwa ni muislamu na atalala hali ya kuwa ni kafiri au atalala hali ya kuwa ni kafiri na ataamka hali ya kuwa ni  muislamu.
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: (Hakika kabla ya kiama kutakuwa na fitna kama kipande cha usiku wa giza mtu ataamka muislamu na atalala kafiri na atalala kafiri na ataamka muislamu na aliyekaa ni bora kuliko aliyesimama na aliyesimama ni bora kuliko aliyetembea na anayetembea ni bora kuliko anayekwenda mbio].

4)   Kudhihiri moto katika ardhi ya Hijazi (Beaking of fire from the land of Hijaz)
 Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): (Hakitasimama kiama mpaka utoke moto katika ardhi ya Hijazi unatoa mwangaza moto huo kiasi utaona shingo za ngamia Basra].

5) Kupotea kwa amana {lose of trust}
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) asema: ( Ikipotea amana ngojea kiama).

6) Kuenea zinaa (spreading of adultery), kiasi kwamba litakuwa jambo la kawaida na asiyejihusisha na jambo hilo watu watamshangaa.
 Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Naapa kwa ambae nafsi yangu iko mkononi mwake hautamalizika umma huu mpaka asimame mwanamume na mwanamke na amlaze njiani afanye nae zinaa aseme mbora wao siku hiyo lau mtazunguka nyuma ya ukuta (mufanyie huko)
.
7) Kuenea kwa riba (spreading of Riba (usury)). Dhambi hii mbaya na ya kuangamiza lakini    namna itakavyoenea litakuwa jambo la kawaida, na watu hawajali na watajaza matumbo yao haramu.
قال تعالى : {وَأَحَلَّ اللَّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا} [البقرة 275]
Mola mlezi amesema:{ Na Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na ameharamisha riba} [Al-Baqara : 275].

Na bwana Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [ kabla ya kuja kiama kutadhhiri riba].

8) Watu kujenga majumba makubwa na marefu (peoples building very huge and tall building)  Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) alipotaja baadhi ya alama za kiama:
[Ni kuzaa mtumwa wa kike bwana wake na utaona watu wasiokuwa na viatu waliouchi, masikini, wachunga mbuzi wanashidana kurefusha majumba].  Na Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: [Hakitasimama kiama mpaka watu wajifakhiri kwa kujenga Misikiti].

10) Kushindana Na Kujisifia Katika Kuipamba Misikiti (Making Competition and proud of among each other for mosques decoration)
 Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
((Katika dalili za kukaribia kwa Qiyaamah ni watu kushindana na kujisifia katika kuipamba misikiti.)) [Imepokewa na An-Nasaaiy]
           
11) Kukithiri uongo baina ya watu (excessive lie among the people)
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema katika hadithi yake:
(Hakitasimama kiama mpaka zidhihiri fitna, kukithiri uongo na kukaribiana masoko).
12) Kutamani mauti kwa yule aliye hai kutokana na hali za watu zitakavyokuwa mbaya (desering death for living person, from the worst conditions people will live)
Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) amesema:
( Hakitasimama kiama mpaka aende alie kaburini asimame aseme natamani mahali pako) yaani atatamani alie hai afe yeye.
 Alama Kubwa za Kiama.

 1) Kutokea kwa Dajjal (Dajjal's Emergence) Huyu ni kiumbe wa ajabu ambaye atawafitini watu na kuwapotosha na kuwatia katika ukafiri. Katika mitihani yake ni kule kuwa kwake na pepo na moto, atakaye muamini yeye atamwingiza peponi na atakaye muasi atamtia motoni. Hatoacha kufanya hivyo mpaka atakapo kuja Nabii Isa, apambane nae na kumuua.

2) Kutokea kwa Yaajuj na Maajuj {appearance of Ya'juj Ma'juj (Gog and Magog)} Hawa ni viumbe wa ajabu  watatokea maeneo ya Asia ya kati walikofungiwa na Mfalme Dhur- Qarnain kutokana na kule kufanya uharibifu wao katika ardhi. Allah anatusimulia;

قال تعالى : {قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ عَلَى أَنْ تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ خَرْجًا سَدًّا}  [الكهف : 94]

Na Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {Wakasema: Ewe Dhul-Qarnain hakika Yaajuj na Maajuj wanafanya uharibifu katika ardhi, basi je tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi}} [Al-Kahfi : 94].
قال تعالى : {حَتَّى إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُمْ مِنْ كُلِّ حَدَبٍ يَنْسِلُونَ} [الأنبياء : 96]
Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema: {Hata watakapofunguliwa Yaajuj na Maajuj wakawa wanateremka kutoka kila mlima}} [Al-Anbiya : 96].

3) Kushuka kwa Nabii Issa {the Descending of Prophet Jesus (A. S) Nae atakuja kupambana na Dajjal na kumuuwa baada yakwisha kuwapoteza watu sana.  
                         
4) Kuja kwa Mahdy {comming of Imam Mahdy} Mtazamo wa wanavyuoni walio wengi {Ahlu sunna waljamaa} kutokana na hadithi zilizo nyingi Imam Mahdi atakuja kabla ya Dajjal, ama dajjal atakuja mwishoni wa kipindi chake.
5) Kuchomoza jua kutoka Magharibi {Rising of the Sun from the West} kipindi cha lala salama ambapo      milango ya toba itafungwa na hatosamehewa mtu yoyote kuomba msamaha wala kurejea tena kwa Mwenyezi Mungu .
                                               
6) Kudhihiri moshi duniani na kutoka mnyama anaezungumza na watu na kuwakumbusha mambo ya Mwenyezi Mungu (appearance of smoke and animal who speaks to the people reminding them about their Lord}
                                
7) Kushikwa jua sehemu tatu {Triple luner eclipses}; kushikwa jua mashariki, magharibi na bara arabu.
8) Kutoka moto sehemu ya Aden {fire appearance from Aden} katika nchi ya Yemen ulio wazi kabisa utakaokusanya watu katika ardhi ya watu kuhesabiwa vitendo vyake.  
Ndugu yangu muumini, hizi ni baadhi tu ya dalili za siku ya vishindo na majonzi, siku ya furaha na huzuni, siku ya karaha na neema. Mwanadamu yupo katika hasara tokea siku ya kukutana kwa yayi la mama na baba,, zingatia mwanadamu, hasara hii kama hutakua makini itakua ni hasara ya hapa duniani hadi kukutana na muumba wako.
Kiyama kipo, na kinakuja, ilhali hakipo mbali japo kuwa walowengi wanaona kipo mbali. Fikiri ulipotoka, hapa ulipo ni wapi, na wapi mafikio yako. Mafikio mwanandani na siku ya kukutana na Muumba wako, tumia fursa hii adhimu na adimu, kabla haijafika siku ambayo majuto hayatakusaidia.

WABILLAH TAWFIIQ.

UNIVERSITY OF DARES SALAAM TANZANIA.




No comments:

Post a Comment