Waislamu
nchini Tanzania wameungana na waislamu wengine duniani kote katika kuadhimisha
siku ya Qudsi duniani kufuatia dhulma zinazoendelezwa na utawala dhalimu wa
Israil unaoendeleza jinai, kuwanyanyasa, kuwatesa na kuwauwa wapalestina wasio
na hatia katika ukanda wa Ghaza.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo, Alhajji Sheikh Aliy Basweleh maarufu kama mzee wa
kunukuu amesema, kinachofanywa na utawala haramu wa Israil ni kitendo cha
kinyama kinachopaswa kukemewa na kila mpenda amani, haki na usawa duniani.
Amesema
kama waislamu wanaalaani vikali dhuma hizo na kamwe hawakotayari kuona utawala
huo dhalimu ukiendelea kuwakandamiza Wapalestina, kuwauwa na kuwamyima uhuru
wao, huku wakiendelea kuivunjia heshima nyumba tukufu na qibla ya kwanza ya
waislamu Masjid Al-aqswa.
Kwa upande
wake Imam Mkuu wa Masjid Ghadir Samahatu Sheikh Mohammed Jalal amesema waislamu
wanatakiwa kuunganisha nguvu yao bila kujali itikadi zao kuhakikisha
wanapambana na dhulma hiyo na kuwa tayari kuukomboa Msikiti Mtukufu wa Aqswa.
Ikumbukwe
kuwa siku ya Qudsi huadhimishwa kila mwaka katika Ijumaa ya mwisho wa Mwezi
mtukufu dwa ramadhani tangu kuasisiwa kwake na Imam Khomein mwasisi wa Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran, kwa lengo la kulaani jinai zinazofanywa na utawala bandia
wa Israel, dhidi ya Wapalestina.
No comments:
Post a Comment