Wednesday, August 27, 2014

HOTUBA YA JAJ. WARIOBA 30 DESEMBA, 2013








HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA
KATIBA, MHE. JOSEPH S. WARIOBA WAKATI WA KUKABIDHI
RIPOTI YA TUME KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE NA
RAIS WA ZANZIBAR MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN;
TAREHE 30 DESEMBA, 2013, DAR ES SALAAM
________________






Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa





Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania;

Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu;


Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar;
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;

Mheshimiwa

Pandu

Ameir

Kificho,

Spika

wa

Baraza

la

Wawakilishi;
Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania;
Mheshimiwa Omar Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar;
Mheshimiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Pili wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;



1






Mheshimiwa Mzee Benjamin Mkapa, Rais wa Tatu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
Waheshimiwa Viongozi wote mliopo hapa;


Waheshimiwa Mabalozi;


Ndugu wananchi;


Mheshimiwa Rais,


Kwa makubaliano na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, tarehe 6 Aprili,

2012 ulituteua kuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,

ulituapisha tarehe 13 Aprili na tulianza kazi tarehe 2 mei, 2012. Tulikuwa

34, yaani wajumbe 32 na Katibu na Naibu Katibu. Leo tuko hapa 32.

Kama inavyofahamika tulimpoteza mjumbe mmoja, Dr. Sengondo Mvungi

katika mazingira ya kusikitisha.Mungu aiweke roho yake mahali pema

peponi. Mjumbe mwingine, ndugu John Nkolo, hayuko hapa kutokana na


matatizo ya kiafya.

Hali yake inaendelea vizuri.

Vile vile mjumbe wa


sekretariati ndugu Onorius Njole aliugua wakati Tume ilipokuwa

inasimamia Mabaraza ya Katiba. Naye pia hali yake inaendelea vizuri.


Mheshimiwa Rais,


Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa miezi kumi na nane kwa Tume


kukamilisha kazi yake.

Sheria pia ilitoa nafasi ya Tume kuongezewa


muda usiozidi miezi miwili na Tume iliomba muda huo na ulitukubalia.


2






Kazi tuliyopewa tumeikamilisha na leo tupo tayari kukabidhi kwako

na kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar Ripoti yetu kama sheria


inavyoelekeza.

zifuatazo:-

Ripoti tunayoikabidhi inaambatana na taarifa saba



(i)





(ii)


Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania;

Maoni ya Mabaraza ya Katiba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri


ya Muungano wa Tanzania;

(iii) Maoni ya Wananchi kuhusu Sera, Sheria na Utekelezaji;

(iv) Takwimu za Ukusanyaji wa maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko

ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(v) Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania;

(vi) Viambatisho vya Ripoti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba; na

(vii) Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mheshimiwa Rais,


Kabla ya kukabidhi Ripoti yetu naomba univumilie niweze kusema

machache lakini kwa maneno mengi. Napenda kuanza na shukrani. Baada

ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukamilisha kazi hii,

shukrani zetu kwanza ni kwako Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais wa



3






Zanzibar.

mliotupa.





Tunawashukuru kwa kututeua na pia kwa msaada mkubwa

Kila tulipokwama mahali mlikuwa wepesi kutoa maagizo


yaliyotukwamua.

Tunawashukuru sana Mawaziri wa Katiba na Sheria,


Wanasheria Wakuu wa Serikali, Makatibu Wakuu Viongozi na Watendaji

Wakuu wa Wizara za Katiba na Sheria, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa

Wilaya, Wakurungenzi na Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,

Watendaji wa Tarafa, Kata na Shehia, Vijiji na Wenyeviti wa Serikali za


vijiji kwa ushirikiano mzuri walioutoa kwa Tume.

Aidha, Tume inatoa


shukrani za dhati kwa Jeshi la Polisi na Kamati za Ulinzi na Usalama za

Wilaya kwa kuhakikisha mchakato mzima unakamilika kwa usalama.


Tume pia inatoa shukrani kwa Vyama vya siasa, Jumuiya za Dini,

Asasi za Kiraia, Taasisi na makundi mengine kwa mchango wao. Kwa

namna ya pekee, tunavishukuru vyombo vya habari ambavyo, licha ya


kusambaza

taarifa

mbalimbali

zilizokuwa

zikitolewa

na

Tume,


vimeuelimisha Umma na kuufanya mchakato mzima wa katiba kuwa wa

wazi na wenye hamasa.


Mwisho kwa uzito wa pekee Tume inawashukuru wananchi, hasa

wananchi wa kawaida, kwa mchango wao mkubwa wa mawazo na maoni.

Hii ni mara ya kwanza katika nchi yetu kwa wananchi wa kawaida

kushiriki katika kutoa maoni kuhusu aina ya Katiba wanayoitaka na

wamefanya hivyo kwa wingi na kwa uzito mkubwa.

4






Mheshimiwa Rais,


Kama nilivyosema mapema, pamoja na Ripoti ya Tume kuhusu

mchakato wa katiba ambayo tunakabidhi leo, tunakabidhi pia na Rasimu

ya Katiba. Rasimu hiyo ni ndefu kuliko Rasimu ya awali. Rasimu ya awali

ilikuwa na ibara 240. Rasimu ya sasa ina ibara 271. Ongezeko la ibara

kwa kiwango kikubwa limetokana na Tume kuzingatia maoni ya Mabaraza

ya Katiba. Muhtasari wa Rasimu uko kwenye Sura ya Kumi na Mbili ya

Ripoti yetu. Kwa leo nitagusia mambo machache ambayo Tume imeona

vyema tukatoa maelezo.


Jambo la kwanza, ni ushiriki wa wananchi katika mchakato mzima

wa kupata katiba mpya. Tume ilipoanza kulikuwa na wasiwasi kwamba

ushiriki wa wananchi wa kawaida ungekuwa dhaifu kwa sababu iliaminika

kwamba wananchi kwa ujumla wao hawana ujuzi wa katiba. Lakini Tume

iligundua mapema kwamba wananchi wanajua mambo mengi ambayo ni

msingi wa katiba yoyote ile.


Sura tano za mwanzo za Rasimu ya Katiba zinatokana na mchango

mkubwa kutoka kwa wananchi, hasa kuhusu Misingi ya Taifa, Tunu za

Taifa, Maadili na Miiko ya Uongozi, Dira ya Taifa na Haki za binaadam.

Wananchi pia wametoa maoni mazito kuhusu uongozi na utawala wa

nchi, ikiwa ni pamoja na nafasi ya wawakilishi wao Bungeni.



5






Hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwashirikisha kwa ukamilifu

wananchi katika kutunga katiba ya nchi yao. Nia ya mchakato huu ni

kupata katiba inayokubalika na wananchi. Ili katiba ikubalike na wananchi

ni jambo la msingi maoni yao yapewe uzito unaostahili. Nayasema haya

kwa sababu tangu Rasimu ya kwanza itolewe maeneo yaliyopewa uzito

na wananchi hayakupewa uzito katika mijadala ya viongozi, wasomi na

vyombo vya habari.


Mheshimiwa Rais,


Utangulizi wa Katiba unaeleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania imetungwa na Wananchi wa Tanzania. Utangulizi

unatoa taswira na picha halisi ya Jamhuri ya Muungano na watu wake,

historia yao, matarajio yao, misingi ya taifa na masuala muhimu ambayo

Wananchi wanataka kuyaendeleza katika jamii, kizazi hadi kizazi.


Sura ya Kwanza inaelekeza kuendelea kuwepo kwa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania. Yapo pia masharti kuhusu alama za Taifa na

sikukuu za Taifa na Rasimu inatambua Lugha ya Kiswahili kuwa Lugha ya


Taifa.

Imeainisha pia tunu za Taifa ambazo ni Uhuru, Haki, Udugu,


Amani, Usawa, Umoja na Mshikamano. Tunu za Taifa ndiyo msingi wa

maadili na taratibu mbalimbali za kimaisha za jamii mbali mbali ambazo

hurithishwa kizazi hadi kizazi.



6






Mheshimiwa Rais,


Dira ya Taifa ni eneo ambalo wananchi walilitolea maoni kwa wingi

na kwa uzito. Sura ya Pili ya rasimu kuhusu malengo muhimu, misingi ya

mwelekeo wa shughuli za Serikali na sera za kitaifa imejumuisha maoni

mengi ya wananchi. Wakulima, wafugaji, wavuvi na makundi mengine

wanataka kuwe na dira ya Taifa ambayo ndiyo itakuwa mwongozo mkuu

utakaofuatwa na kuzingatiwa na uongozi, hasa Serikali na vyama vya

siasa katika kutekeleza shughuli za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni

na kimazingira.


Sura ya Tatu imependekeza masharti kuhusu Maadili na Miiko ya

Uongozi na Utumishi wa Umma. Uongozi ni dhamana, na kiongozi wa

Umma anatakiwa kutekeleza wajibu wake kwa kuheshimu Wananchi,

kukuza hadhi ya Taifa na kukuza imani na heshima ya Utumishi wa Umma

kwa Wananchi. Rasimu imeorodhesha miiko ya uongozi ikiwa ni pamoja

na kupiga marufuku kiongozi wa Umma kutumia wadhifa, nafasi ya

madaraka au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu,

jamaa, marafiki au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu.


Mheshimiwa Rais,


Sura ya Nne, inahusu Haki za Binadamu, Wajibu wa Raia na


Mamlaka za Nchi.

Wananchi wametoa maoni mengi kuhusu haki za


7






binadamu na hasa katika suala la utekelezaji na usimamizi wa haki hizo.

Kutokana na maoni ya Wananchi, Rasimu imeboresha haki za binadamu

zilizomo katika Katiba ya sasa na kuongeza haki mpya za mtu binafsi na

haki za makundi mbalimbali kama vile watoto, wanawake, wazee, vijana,

makundi madogo katika jamii, watu wenye ulemavu, wafanyakazi, waajiri


na haki ya kutafuta, kutoa na kusambaza habari.

Aidha, Rasimu


imeainisha wajibu wa raia ikiwa ni pamoja na kulinda na kutetea Katiba

na Sheria za Nchi; kulipa kodi, kuheshimu haki, uhuru na maslahi ya watu

wengine na kulinda na kutunza mazingira.


Sura ya Tano inahusu Uraia wa Jamhuri ya Muungano. Uraia ni

mmoja, nao ni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rasimu ya Katiba

inapendekeza kutambuliwa kwa uraia wa kuzaliwa na kujiandikisha


ambao ni wa nchi moja.

Aidha, Rasimu inapendekeza kuwapa hadhi


maalum watu wenye asili au nasaba ya Tanzania ambao wameacha kuwa

raia wa Tanzania kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine.


Mheshimiwa Rais,


Kuhusu Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Rasimu ya Katiba

imefafanua kwa kina na ufasaha juu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano

ambaye ni alama na taswira ya nchi na Watu wake. Yeye peke yake

ndiye mwenye hadhi na heshima ya Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu na



8






Kiongozi wa Serikali. Kwa kuzingatia maoni ya Wananchi, madaraka ya

Rais na hasa yale ya uteuzi yamepunguzwa kwa kuweka vyombo vya

kupendekeza majina ya Watu wa kuteuliwa na kwa baadhi ya vyeo

kuhitaji kuthibitishwa na Bunge.


Mheshimiwa Rais,



Wananchi wametaka Katiba itambue mamlaka na madaraka


yao


juu ya wawakilishi wao katika Bunge, na kama ilivyokuwa katika Rasimu

ya Awali, inapendekezwa Wabunge wasiwe Mawaziri, kuwe na ukomo wa

uwakilishi katika Bunge na wapiga kura wawe na madaraka ya

kumwajibisha Mbunge hata kabla ya kumalizika kwa muhula wake na

Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge au kiongozi wa juu wa

chama cha siasa.


Kuhusu Mahakama ya Jamhuri ya Muungano, Sura ya Kumi imebaki

na mapendekezo ya awali ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu

(Supreme Court) na kuendelea kuwepo kwa Mahakama ya Rufani. Aidha,

inapendekezwa, kama ilivyo katika Katiba ya sasa, Mahakama Kuu ya

Tanzania Bara (Tanganyika) na Mahakama Kuu ya Zanzibar, ziendelee

kuwa na mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali, mashauri ya

madai na jinai yanayohusu sheria za Serikali ya Jamhuri ya Muungano

katika maeneo yao ya utawala (concurrent jurisdiction).



9






Mheshimiwa Rais,


Tume kwa kuzingatia maoni ya Wananchi, tofauti na ilivyokuwa

katika Rasimu ya Awali, sasa inapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa

iwe ni taasisi inayojitegemea na siyo kuwa Sehemu ya Tume Huru ya

Uchaguzi.


Kuhusu ulinzi na usalama, Sura ya Kumi na Tano inatamka kuwa

jukumu la ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano ni la kila raia.

Kwa kuzingatia maoni ya Wananchi waliyoyatoa katika Mabaraza ya

Katiba, Rasimu sasa inapendekeza kuwepo kwa Jeshi la Polisi moja na

Idara ya Usalama wa Taifa moja katika Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania.


Mheshimiwa Rais,


Mabadiliko makubwa ya Katiba lazima yaendane na masharti

yatokanayo na Masharti ya Mpito ambayo nayo ni sehemu ya Katiba.

Masharti haya yanaweka utaratibu, mfumo wa kikatiba na kisheria kuhusu

masuala ya kiutawala, uongozi wa nchi, sheria za nchi, nafasi za

madaraka na namna mambo yote hayo yatakaavyokuwa na kuendeshwa.


Sura ya Kumi na Saba inapendekeza Muda wa Mpito wa Miaka

Minne, kuanzia tarehe ya kuanza kutumika kwa Katiba Mpya hadi tarehe


31 Desemba, 2018.

Katika kipindi hicho, sheria zilizopo hivi sasa

10






zitaendelea kutumika hadi zitakapobadilishwa.





Sheria zinazotumika


Tanzania Bara zitakuwa za Tanganyika na sheria zinzotumika Tanzania

Bara na Zanzibar zitakuwa Sheria za Jamhuri ya Muungano. Yapo pia

mapendekezo kuhusu masuala ya kufanyiwa kazi katika Muda wa Mpito.

Mambo haya ni pamoja na:-



(i)

(ii)








(iii)





(iv)








(v)








(vi)


Kutungwa kwa Katiba ya Tanganyika;

Kurekebisha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 ili kuwiana

na masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania ya mwaka 2014;

Mgawanyo wa rasilimali baina ya Serikali ya Jamhuri ya

Muungano na Serikali za Nchi washirika;

Kuundwa kwa Tume na Taasisi za Kikatiba zilizoainishwa

kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya

Mwaka 2014 na kwa kuzingatia masharti ya Katiba hiyo;

Kufanya maandalizi na kuendesha Uchaguzi Mkuu wa

Mwaka 2015 kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri

ya Muungano ya Mwaka 2014; na

Kufanya maandalizi ya mambo yote muhimu kwa ajili ya

utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba yaliyomo kwenye

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka

2014.


11






Mheshimiwa Rais,


Moja ya mambo ambayo yamejadiliwa sana na kwa hisia kali tangu


Rasimu ya awali ilipotolewa na Tume ni Muungano wa Tanzania.

Jambo


kubwa limekuwa juu ya muundo wa Muungano. Wakati Tume inazindua

Rasimu ya Awali tulisema hatukupendekeza kuendelea kuwa na muundo

wa Serikali mbili kwa sababu mbalimbali. Tulisema kuwa kuendelea kwa

Serikali mbili kulihitaji ukarabati mkubwa ambao tulifikiri hautawezekana.

Mabaraza ya Katiba yalitoa maoni mengi ambayo yaliilazimu Tume


kufanya tena uchambuzi wa kina.

Kama ilivyokuwa katika Rasimu ya


Awali, suala la muundo wa Muungano ndilo lililochukuwa muda mwingi

wa Tume. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilielekeza kwamba Tume

itaongozwa na misingi mikuu ya kitaifa na maadili ya jamii ya kuhifadhi na

kudumisha mambo kadhaa. Moja ya mambo hayo ilikuwa ni kuwepo kwa


Jamhuri ya Muungano.

Hivyo, Tume ilianza kazi kwa madhumuni ya


kupata maoni ya kuboresha Muungano. Wananchi wengi walitoa maoni

kuhusu Muungano, lakini wengi wao walijikita kwenye Muundo wake.

Kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu

Muungano na kati ya hao, karibu 27,000 walizungumzia muundo. Kwa

Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwenye suala la


Muungano.

Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni Wananchi


19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano.


12






Mchanganuo wa takwimu hizi unaonyesha kuwa kwa upande wa

Tanzania Bara, 13% walipendelea Serikali moja, 24% walipendekeza


Serikali mbili na 61% walipendekeza Serikali tatu.

Kwa upande wa


Zanzibar, 34% walipendekeza Serikali mbili na 60% walipendekeza

Muungano wa Mkataba, na 0.1% (watu 25) walipendekeza Serikali moja.

Aidha, taasisi nyingi kama vile vyama vya siasa, asasi za kiraia na jumuia


za kidini zilipendekeza muundo wa Serikali tatu.

Baadhi ya taasisi za


kiserikali, ama moja kwa moja au kwa tafsiri ya mapendekezo yao, pia

zilipendekeza Serikali tatu. Kwa mfano, Baraza la Wawakilishi Zanzibar

lilipendekeza kuwepo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya

Tanganyika na mamlaka ya Muungano na iwekwe wazi maeneo, uwezo,


nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka.

Ofisi ya Waziri Mkuu


imependekeza mfumo wa serikali tatu ili kuondoa kero za muungano.

Aidha, Mamlaka ya Mapato Tanzania imependekeza kuwepo kwa Serikali

tatu ili kutoa majibu ya kero zilizopo na kuleta utulivu zaidi ilimradi

upangiliwe vizuri.


Mheshimiwa Rais;


Baada ya kuona takwimu hizi na kuchanganua sababu zilizotolewa

na makundi mbali mbali, Tume iliamua kufanya utafiti kuhusu muundo wa

Muungano. Suala hili lilijitokeza kwa nguvu na hisia kali mara ya kwanza

mwaka 1984 katika kipindi kilichoitwa “kuchafuka kwa hali ya hewa

13






kisiasa Zanzibar”. Mwaka 1991 Tume ya Nyalali ilipendekeza Muundo wa


Serikali tatu.

Miaka miwili baadaye, yaani Mwaka 1993, kikundi cha


Wabunge

wa

Tanzania

Bara

katika

Bunge

la

Muungano,

G55,


kilipendekeza kuwa na muundo wa Serikali tatu na Bunge likaridhia.

Mwaka 1999 Kamati ya Kisanga ilipendekeza muundo wa Serikali tatu.

Tume pia imepitia taarifa ya Kamati nyingi zilizoundwa na Serikali ya

Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama vile,

Kamati ya Amina Salum Ali na Kamati ya Shelukindo ya mwaka 1994.


Sababu zilizotolewa katika matukio hayo ya mwanzo kwa kiwango

kikubwa, zinafanana na zile ambazo zimetolewa kipindi hiki. Kila upande

wa Muungano una malalamiko mengi kuhusu muundo wa Muungano.

Katika Taarifa ya Tume tunayokukabidhi leo, tumeorodhesha malalamiko

kumi kwa upande wa Zanzibar na malalamiko manane kwa upande wa

Tanzania Bara. Kwa upande wa Zanzibar malalamiko matatu makubwa

ni;



(i)








(ii)


Serikali ya Tanganyika imevaa koti la Serikali ya Muungano

ambalo linaisaidia Tanganyika zaidi kuliko Zanzibar. Koti hilo

limeifanya Tanganyika kuwa ndiyo Tanzania;

Mambo ya Muungano yamekuwa yakiongezeka na hivyo

kuathiri madaraka ya Zanzibar (autonomy) na kufifisha hadhi

ya Zanzibar (identity) na Zanzibar inaendelea kumezwa; na
14






(iii)





Kumwondoa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa


Jamhuri ya Muungano.


Kwa upande wa Tanzania Bara, malalamiko makubwa ni;



(i)


Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo

wake wa Taifa ina Serikali yake na imebadili Katiba yake ili

ijitambue kama nchi, wakati Tanzania Bara imepoteza


utambulisho wake.

Katiba ya Jamhuri inasema Tanzania ni


nchi moja lakini Katiba ya Zanzibar inasema ni nchi mbili;


(ii)















(iii)

Zanzibar imebadili Katiba yake na kuchukua madaraka ya

Jamhuri ya Muungano, kama vile kuelekeza sheria za

Muungano zilizopitishwa na Bunge la Muungano zipelekwe

kwenye Baraza la Wawakilishi. Maana yake ni kuwa Katiba ya

Zanzibar sasa ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano; na

Wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki


ardhi Zanzibar wakati wenzao wa Zanzibar wana haki hiyo

Tanzania Bara.


Mheshimiwa Rais;


Katika kuchambua malalamiko ya Zanzibar kwamba Tanganyika

imevaa koti la Muungano, Tume imebaini kwamba muundo wa Muungano

wa Serikali mbili umeifanya Serikali ya Muungano kwa kiwango kikubwa


15






kushughulikia zaidi mambo ya Tanzania Bara, hasa mambo ya

maendeleo. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka

1977, Serikali ya Muungano ina mamlaka ya kusimamia mambo ya

muungano na mambo yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanzania

Bara. Kwa msingi huo, Serikali ya Muungano inashughulikia sana mambo

ya kilimo, elimu, afya, maji, nishati na madini, ujenzi, uchukuzi, maliasili

na utalii na mengine ya Tanzania Bara ambayo siyo mambo ya

Muungano. Wakati wa kikao cha Bajeti Bunge la Muungano hutenga siku

mbili au tatu za majadiliano kwa Wizara zinazosimamia mambo haya

yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara wakati mambo ya Muungano kama

vile ulinzi, mambo ya nje na mambo ya ndani hutengewa siku moja au


nusu siku.

Maswali ya Wabunge kuhusu mambo ya maendeleo pia


yanahusu Tanzania Bara na ziara za Wabunge kukagua miradi ya

maendeleo zinahusu Tanzania Bara katika mambo yasiyo ya Muungano.

Mambo haya Bungeni yanasimamiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya

Muungano ambaye, kihalisia hana mamlaka wala madaraka yoyote

kuhusu Zanzibar.


Aidha, muundo huu wa muungano pia umesababisha kuwepo kwa

wizara au taasisi zenye sura au zinazotekeleza mambo ya muungano

pekee; mambo ya Tanzania Bara na mambo mchanganyiko; kwa maana

ya mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano, hali ambayo


16






inapekea ugumu wa kutofautisha gharama za muungano na zisizo za

muungano katika wizara au taasisi hizo. Kundi la pili na la tatu ndio

imekuwa chanzo cha kero za muungano.


Hakuna njia ya kubadili hali hii kwa sababu Serikali ya Muungano

haina mamlaka ya kutosha juu ya mambo ya maendeleo kwa upande wa


Zanzibar.

Mawaziri wengi na Serikali kwa ujumla inalazimika kupanga


maendeleo na kutafuta rasilimali kwa ajili ya Tanzania Bara zaidi kuliko

kwa Zanzibar. Zanzibar hufanya mipango yake ya maendeleo. Lakini, ili

kupata rasilimali kama mikopo na misaada ni lazima ipitie Serikali ya

Muungano, jambo ambalo utekelezaji wake umesababisha matatizo

mengi. Utatuzi wa matatizo hayo umekuwa mgumu, umechukua muda

mrefu au umeshindikana. Njia pekee ambayo ingefanya maendeleo ya

Zanzibar yapewe uzito sawa na mambo ya Tanzania Bara ni kuyaweka

mambo hayo chini ya Serikali ya Muungano, yaani kuwa na Serikali moja.

Hata hivyo, hilo likifanyika kuna hofu ya Zanzibar kumezwa.


Mheshimiwa Rais;


Tume imefanya uchambuzi wa ndani kuhusu malalamiko ya

Zanzibar kwamba kuongezeka kwa Mambo ya Muungano kumeathiri

madaraka ya Zanzibar (autonomy). Tangu mwanzo wa Muungano,

ilikubalika kwamba Zanzibar ibaki na hadhi yake na iwe na madaraka



17






kuhusu Mambo yasiyo ya Muungano. Tume ilifanya uchambuzi wa Mambo

ya Muungano ili kubaini kama yanaingilia hadhi na uhuru wa Zanzibar.

Kati ya Mambo 22 ya Muungano, Tume imebaini kuwa siyo mambo yote

yanatekelezwa kikamilifu kimuungano. Mambo mengi yamebadilishwa bila

ya kubadili katiba, ama kwa makubaliano kati ya pande zote mbili za

Muungano au kwa hatua zilizochukuliwa na upande mmoja. Mambo hayo

ni pamoja na kodi, bandari, leseni za viwanda, usafiri na usafirishaji wa

anga, utafiti, posta na simu, uraia, takwimu, mafuta na gesi na

Mahakama ya Rufani.


Kwa hali halisi ilionekana hakuna uwezekano kuyarudisha kwenye

orodha ya muungano mambo ambayo yameondolewa kiutekelezaji.


Kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita, Kamati nyingi zimeundwa na

kutoa mapendekezo ya kuondoa mambo mengi zaidi kutoka kwenye

Orodha ya Mambo ya Muungano, ikiwa ni pamoja na elimu ya juu,

biashara ya nje, uhusiano wa kimataifa, mikopo, misaada ya nje na

mafuta na gesi. Wakati Tume inakusanya maoni, Wananchi wengi wa

Zanzibar kutoka makundi mawili makubwa, yaani wale waliotaka

Muungano wa Serikali Mbili na wale waliotaka Muungano wa mkataba,

wote walipendekeza mambo hayo yaondolewe kwenye Orodha ya Mambo

ya Muungano.




18






Kwa tathmini ya Tume baadhi ya mambo haya hakuna budi

yaondolewe kutoka orodha ya muungano la sivyo kero za muungano

zitaendelea. Kwa mfano suala la uhusiano wa kimataifa likiendelea kuwa

ni jambo la muungano Zanzibar haitaweza kujiunga na mashirika kama

OIC na FIFA. Kwa msingi huo, Tume imependekeza kuliondoa suala la

uhusiano wa kimataifa katika mambo ya muungano na kubakisha suala la

mambo ya nje.


Eneo jingine ni mgongano kati ya Katiba ya Muungano, na Katiba ya

Zanzibar. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imeweka masharti kwamba

sheria zinazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano hazitatumika

Zanzibar hadi zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi. Aidha, kodi

itakayoamuliwa na Bunge kutozwa na Serikali ya Muungano lazima ipate

ridhaa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


Mambo haya yameleta mgongano wa Katiba. Juhudi zilizofanywa


na pande zote mbili hazikufanikiwa kuondoa mgongano huo.

Zaidi ya


hapo, mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanywa mwaka 2010

yametamka wazi kwamba Zanzibar ni nchi kati ya nchi mbili za Muungano


wakati Katiba ya Jamhuri inaelekeza kwamba

Tanzania ni Nchi moja.


Mabadiliko katika Katiba ya Zanzibar pia yamehamisha baadhi ya

madaraka ya Serikali ya Muungano kwenda Zanzibar.




19






Wakati wa kukusanya maoni ya wananchi, Tume ilibaini kwamba

haitakuwa rahisi kubadili Katiba ya Zanzibar kuifanya Zanzibar kuonekana

kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa sura ya nchi

kamili. Mabadiliko ya aina hiyo yatahitaji kura ya maoni kama Katiba ya

Zanzibar inavyoelekeza. Kwa tathmini ya Tume, baada ya kuwasikiliza

wananchi wa Zanzibar, ni dhahiri kwamba pendekezo la kuifanya Zanzibar

isionekane kama nchi halitakubalika kwenye kura ya maoni.


Kwa kifupi tathimini yetu ni kwamba ukarabati mkubwa unahitajika


ili kuendelea na muundo wa Serikali mbili.

Maeneo mawili makubwa


yanahitaji mabadiliko. Jambo la kwanza ni kuwa na mambo ya kutosha

kwenye orodha ya muungano, ikiwa ni pamoja na mambo ya maendeleo

na kiuchumi. Jambo hilo likifanyika, litazidisha malalamiko kwa upande

wa Zanzibar kuwa hadhi na madaraka yake yanazidi kupotea. Aidha,

Mambo ya muungano yakipunguzwa sana Serikali ya Muungano itakuwa

inashughulika zaidi na zaidi na mambo ya Tanganyika; na Zanzibar itaona

Tanganyika ndiyo muungano. Lakini kwa upande mwingine, Tanganyika

nayo itaona si haki nayo isiwe na uhuru wa kuendesha mambo yake kama

ilivyo kwa Zanzibar.


Jambo la pili ni kuondoa mgongano na mgogoro wa Katiba. Hiyo

maana yake ni Zanzibar kubadili Katiba yake ili Zanzibar na Tanganyika

ziwe ni sehemu za nchi moja badala ya kuwa nchi kamili. Kama Zanzibar

20






na Tanganyika zikiwa nchi kamili haitawezekana nchi moja ikawa na

hadhi na uhuru wake na nchi nyingine isiwe na hadhi na uhuru

(autonomy) wake.


Kwa tathimini ya Tume, kwa hali halisi, tunaona ukarabati huo ni

mgumu. Hii ndiyo sababu kubwa ya kupendekeza muundo wa Serikali

tatu ili pande zote mbili ziwe na hadhi sawa. Kila upande utashughulikia

mambo yasiyo ya muungano na Serikali ya Muungano itabaki na mambo

machache ya msingi na ambayo yanaunganisha taifa.


Mheshimiwa Rais;


Wakati muundo wa Serikali tatu unaonekana kukidhi matakwa ya

watanzania walio wengi na pia kushughulikia ipasavyo mengi ya matatizo

ama malalamiko au kero za Muungano, Tume imetambua kuwa muundo

huo nao una changamoto zake. Ili kujikinga na changamoto hizo Tume


imependekeza mambo matatu.

Jambo la kwanza ni uraia.

Tume


imependekeza uraia uwe mmoja na raia wote wa Jamhuri wawe huru na

wawe na haki zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi nzima


isipokuwa katika mazingira maalum.

Haki zao zikiingiliwa na upande


wowote bila sababu maalum itapelekea kuibuka kwa utaifa; Utanganyika

au Uzanzibari, na uzalendo utayumba. Uzalendo ukiyumba na muungano

pia utayumba.



21






Pili ni Serikali ya Muungano kuwa na uhakika wa mapato kwa ajili ya

kulipia gharama za Muungano. Tume imependekeza ushuru wa bidhaa

uwe ni kodi ya Muungano. Kodi hii itakidhi sehemu kubwa ya matumizi

ya Muungano na sehemu itakayobaki itapatikana kutokana na mapato

yasiyo ya kodi yanayotokana na mambo ya muungano, michango ya Nchi


Washirika na mikopo.

Tatu ni kuundwa kwa Tume ya Uhusiano na


Uratibu wa Serikali chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Muungano

na itajumuisha viongozi wakuu wa nchi washirika. Majukumu ya Tume

hiyo ni kusimamia mashauriano na mashirikiano kati ya Serikali ya

Muungano na Serikali za nchi washirika ili kuhakikisha sera zinawiana na

pia kusimamia na kuimarisha masuala yenye maslahi kwa taifa na pia

kutatua migogoro.


Mheshimiwa Rais;



Kazi hii haikuwa rahisi hata kidogo.


Sisi wajumbe kila mmoja


tulikuwa tumetoka kwenye makundi tofauti tofauti.

Kila mmoja wetu


alikuwa na imani yake, maono yake, itikadi yake, msimamo wake na

kadhalika. Lakini tulikubaliana mapema kabisa kwamba wajibu wetu ni


kwa taifa.

Kwa hivyo, tuliacha imani na misimamo yetu binafsi na


kuamua kuwasikiliza wananchi kwa makini sana.

Majadiliano yetu


yalilenga kupata mwafaka wa kitaifa.

maridhiano.

22

Matokeo yake ni maamuzi ya






Baadhi ya mapendekezo yetu kwa hakika yatapokelewa kwa

hamasa kubwa. Lakini la muhimu ni kupata mwafaka wa kitaifa badala

ya kufikia uamuzi kwa kujipima katika makundi.


Baada ya kusema hayo machache lakini kwa maneno mengi, kwa

heshima kubwa, naomba sasa kwa niaba ya Tume, kama sheria

inavyoelekeza, nikukabidhi wewe Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Rais


wa Zanzibar, Ripoti

ya Tume pamoja na Viambatanisho

vyake Saba,


ikiwemo Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.













































23