DAR ES SALAAM
Waislamu wametakiwa kuyaendeleza mafundisho ya
safari tukufu ya Mtume Muhammad (SAW) ya Israa na Miiraj.
Akizungumza na Radio Kheri, Drt. Aqiil Mohammed
Aqiil amesema waislamu wanapaswa kuyachukua mafundisho ya safari hio adhimu,
ikiwa ni pamoja na subra hasa katika kuelekea mwezi mtukufu wa ramadhani.
Amesema safari hiyo ni muhimu hasa kutokana na
zawadi ya Swala tano ambazo ndio msingi mkuu wa Uislamu.
Amesema, mtume Muhammad (SAW) licha ya kupata
maudhi mengi kutoka kwa makafiri, kuondokewa na nguzo zake muhimu katika maisha
yake bwana Abuu Twalib na Mke wake Bi khadija, lakini aliendelea kumtegemea
allah (SW) hati hatma ya maisha yake.
Aidha Drt Aqiiq ametumia fursa hiyo kuwaasa
waislamu kuzidisha matendo mema, mapenzi, umoja na mshikamano hususan katika
kuelekea mwezi Mtukufu wa ramadhani.
No comments:
Post a Comment