ZANZIBAR.
Majaji mjini Zanzibar wameendelea kuilalamikia
serikali kutokana na kuondolewa kwa ulinzi wa jeshi la polisi nyumbani kwao
jambo wanalodai linahatarisha uhai wa maisha yao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Mkuu
wa Zanzibar, Omar Othman Makungu amethibitisha kuwapo kwa hali na kusema kuwa mamlaka husika imeanza kufuatilia.
Aidha, Jaji Makungu amesema awali waliwahi
kujadili juu ya suala hilo na kufikia hatua nzuri ambapo, vikosi maalumu vya
SMZ ndiyo vingepaswa kufanya kazi hiyo.
Naye, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar
Makame amesema ni kweli kwamba askari wa
Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) ambao walikuwa wakihusika na shughuli hizo
wameshaondolewa kwenye shughuli za ulinzi
Hata hivyo, amesema tayari wameshapeleka
mapendekezo yao kutaka kila nyumba ya jaji kujengwa kibanda maalumu kwa ajili
ya walinzi, lakini jambo hilo halijafanyiwa kazi hadi sasa.
No comments:
Post a Comment