Idadi
ya Waislamu nchini Canada imeongezeka na kufikia karibu milioni moja na laki
moja.
Matokeo
ya utafiti mpya uliofanywa nchini humo yameonyesha kuwa jamii ya Waislamu huko
Canada huwenda ikawa mara tatu zaidi katika kipindi cha miaka 20 ijayo.
Uislamu
ni dini ya pili kwa ukubwa huko Canada baada ya dini ya Kikristo na ni ya
kwanza katika dini zinazoenea kwa kasi nchini humo.
Kituo
cha sensa ya watu nchini Canada kimetangaza kuwa, ni Waislamu 13 pekee wa Ulaya
ndio walikuwepo huko Canada wakitokea Bosnia-Herzegovina, miaka minne baada ya
kuundwa nchi hiyo mwaka 1867.
Licha
ya vyombo vya habari vya Magharibi kuendesha propaganda kubwa za kueneza chuki
na hofu dhidi ya Uislamu, lakini hali hiyo imeshindwa kuzuia mvuto wa dini hiyo
nchini humo.
Aidha,
licha ya kuwepo vitendo vya kufurutu mpaka vinavyofanywa na watu wasio na
uelewa sahihi wa Uislamu na hivyo kuathiri mtazamo wa walimwengu juu ya dini
hiyo, lakini yote hayo hayajaweza kupunguza mvuto na ongezeko la watu wanaoamua
kuingia katika dini Tukufu ya Uislamu
Hii imekuja
kutokana na takwimu kuonyesha kuwa Uislamu ndiyo dini inayokua kwa kasi zaidi
katika nchi za Magharibi.
No comments:
Post a Comment