
Mtandao wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Nia ya utafiti huo ilikuwa ni kujua kama wateja
wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana
na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Aidha, utafiti huo umeohusisha takribani watumiaji
700,000 na unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili
kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai
hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na
mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
Waziri wa kazi Jim Sheridan mjumbe wa bodi ya
mawasiliano ameagiza uchunguzi kufanyikadhidi ya mtandao huo wa Facebook katika
tuhuma hizi.
Hata hivyo Katherine Sledge Moore, Profesa wa
Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois amesema kwa jinsi ambavyo
Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo
katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa
taarifa ya utafiti huo amesema wanadhani kuwa ilikuwa mhimu kwao kutafiti
mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao
na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .
No comments:
Post a Comment