Wizara
ya Afya Zanzibar imezindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa
ni mikkati ya kuhakikisha ugonjwa wa malaria unatokomezwa Zanzibar.
Akizindua
mpango hou, Waziri wa wizara hiyo, juma Duni Haji kukamilika kwa ugawaji wa
vyandarua hivyo kunaweza kutokomeza moja kwa moja ugonjwa wa malaria ambao kwa
Zanzibar upo chini ya asilimia moja.
Amesema
licha ya maambukizi kuwa chini ya asilimia moja, lakini mikakati ya wizara ni
kuhakikisha ugonjwa huo unabaki kuwa historia katika visiwa vya Zanzibar.
Amesema
jumla ya vyandarua laki tatu na kumi na tano elfu mia nne sitini na tano
(315,465) vinatarajiwa kugawiwa kwa wakazi wa Unguja na Pemba.
Kwa upande
wake Msaidizi Meneja wa kitengo cha kupambana na malaria Zanzibar Mwinyi Mselem
amesema pamoja na kutoa vyandarua hivyo, kitengo chake pia kinaendelea na
upigaji dawa kwa ajili ya kuuwa mazalio ya mbu wa malaria.
No comments:
Post a Comment