Raisi
wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Msisho Kikwete amesema,
Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha inapunguza vifo vinavyotokana na
saratani ya mlango wa kizazi na matiti nchini.
Rais
Jakaya Kikwete amesema hayo wakati akizindua kampeni ya uchunguzi wa awali wa saratani ya mlango wa kizazi na ile ya
matiti uliofanyika kwenye uwanja wa chipukizi Mkoani Tabora.
Aidha,
Rais Kikwete amesema serikali
itahakikisha vifo vitokanavyo na
saratani vinapungua kwa kiasi kikubwa kwani tayari wizara imejipanga kufanya
hivyo.
Aidha
Raisi Kikwete amewasisitiza wanawake nchini
kujitokeza kwa wingi kupima afya zao mara kwa mara angalau mara moja
kila baada ya miaka mitatu kwani saratani inatibika.
No comments:
Post a Comment