Thursday, June 5, 2014

LWAKATARE (CHADEMA) KITANZINI TETEZI ZA UGAIDI NYUMBANI KWAKE



POLISI YADAIWA KUWAKAMATA HOUSE BOYS NA GIRL WA LWAKATARE USIKU HUU WAKIHUSISHWA NA UGAIDI.


Jeshi la Polisi linadaiwa kuvamia usiku huu nyumbani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na kumkamata housegirl wake.

aidha, jeshi hilo la polisi limewakamata wafanyakazi wengine wawili (house boys) wa Lwakatare.

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa, hadi muda mfupi uliopita vijana hao wawili, walikuwa wako Kituo cha Polisi Mbezi huku msichana wa kazi wakizunguka naye kwenye gari la patrol bila kumfikisha kituoni.

Aidha chanzo cha habari kimeeleza kuwa, Jeshi hilo la polisi kituoni hapo halikutaka kutaja sababu hasa za vijana hao kukamatwa, ingawa hatimaye mmoja wa watu walioko kituoni hapo amedaiwa kutoa taarifa na kusema kuwa polisi wanasema mmoja wa vijana hao kesi yake iko Arusha!



No comments:

Post a Comment