Ofisi ya rais wa Afrika kusini imetangaza, Rais Jacob Zuma amelazwa
hospitalini kwa ajili ya vipimo vya afya.
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo imesema madaktari wameridhika na
hali yake, lakini hawakuendelea kutoa taarifa zaidi juu ya nini alichokuwa
akiugua Rais Zuma.
Siku ya Ijumaa Zuma alishauriwa kupumzika baada ya harakati kubwa
za kampeni ya uchaguzi na mpango wa mpito kuelekea utuwala mpya.
No comments:
Post a Comment