Mahakama moja nchini Misri imewahukumu kifo
wafuasi 10 wa chama kilichopigwa marufuku cha Udugu wa Kiislamu cha rais
aliyepinduliwa madarakani Mohammed Mursi.
Aidha, mahakama hiyo imeakhirisha hadi tarehe 5
Julai kutoa hukumu ya kesi inayomkabili kiongozi mkuu wa Ikhwanul Muslimin
Muhammad Badie na watu wengine 38 wakiwemo maafisa wa chama hicho
Kiongozi huyo wa Ikhwanul Muslimin ambaye
tayari ameshahukumiwa adhabu ya kifo katika moja ya kesi zilizofunguliwa dhidi
yake anakabiliwa pia na kesi nyengine zipatazo 40 ambazo nazo pia kama
atapatikana na hatia atahukumiwa adhabu ya kifo.
Kufuatia hukmu ya kifo ya wafuasi hao 10, Jaji
Hassan Fareed ameiwasilisha hukumu hiyo kwa Mufti Mkuu wa Taasisi ya Ngazi ya
Juu ya Kiislamu nchini humo ili iidhinishwe kama inavyotakiwa kisheria.
Wakati huohuo polisi wamewatia nguvuni wafuasi
15 wa Muhammad Morsi, Rais wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani, sambamba na
kukaribia kuapishwa Abdel Fattah el-Sisi kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Kuapishwa kwa El-Sisi kutarejesha tena madaraka
ya utawala nchini Misri mikononi mwa afisa wa juu wa jeshi baada ya kupita
miaka mitatu tu tangu mapinduzi ya wananchi yalipomng’oa madarakani aliyekuwa
raisi wan chi hiyo Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment