SEMANTIKI NA PRAGMATIKI
MAARIFA YA LUGHA NA MAARIFA YA ULIMWENGU
IMEANDALIWA NA MUBARAKA A HAMAD
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Maarifa ya lugha ni elimu ya kupambanua vijengo mbalimbali vya
lugha na kanuni zake kulingana na taratibu za lugha hio. Ulimwengu halisi ni
mukatadha ambao maarifa ya lugha huweza kutumika ili kuleta taathira kama
ilivyokusudiwa na msemaji au mwandishi.
Richmond Thomason (2012) anafafanua maana ya semantiki kwamba ni tawi
la isimu ya lugha linalohusu maana za viyambo vya lugha. Hivyo basi ni kusema
kuwa, semantiki ni utanzu wa isimu unaojishughulisha na maana ya maneno au viyambo
vya maneno katika lugha. Swali kuu katika wanasemantiki ni kuhusu ninini maana
ya maana.
Hata hivyo wanasemantiki hujikita katika kuchunguza maana katika
viwango mbalimbali kama vile; ngazi ya sauti (fonimu), neno, virai, vishazi na
hata sentensi. Tawi hili la isimu limekuwa ni muhimu sana hasa kutokana na
umuhimu wa mazungumzo, kwani ili mazungumzo yaeleweke na ujumbe ufahamike panahitajika
maana. Aidha nivyema ifahamike kuwa
semantiki inajihusisha na maana za maneno kiisimu, kwani maana yake hupatikana
kutokana na muundo wa maneno hayo au maarifa ya lugha husika.
Kwa upande wa pragmatiki
Richmond Thomason (2012), anasema kwamba ni tawi la lugha
linalojihusisha na matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha wa wazungumzaji
walugha husika. Hivyo Thomson anadai kuwa pragmatiki inahusu zaidi mambo
mawili; matumizi na muktadha.
Geoffrey Finch
(2000) anasema kuwa, dhana ya pragmatiki ilivumbuliwa katika miaka ya 1930 na
mwanafalsafa C.W. Morris, na imeanza kujulikana kama tawi tegemezi la isimu
lugha miaka ya 1970 ambapo kabla ya hapo pragmatiki ilihusishwa kama tawi la
kifalsafa, na kufafanuliwa kwa kuzingatia misingi mikuu miwili; matumizi na
muktadha.
Kuanazia miaka
ya 80 wataaklamu walianza kuiangalia pragmatiki kama maana ya msemaji na
tafsiri kilichosemwa, yaani maana ya msikilizaji. Kwa upande wake Yule (1996)
anafafanua dhana ya pragmatiki kwa kusema kuwa ni taaluma inayohusu mahusiano
yaliyopo kati ya maana ya lugha na watumiaji wa mambo hayo.
Betty J. Birner (2012) anasema
kuwa dhana hizi ni dhana zinazoshabihiana. Tofauti
kubwa iliyopo kati ya dhana hizi bado ni mjadala mpana kwa baadhi ya wanaisimu
wa lugha, hii ni kwa sababu, pragmatiki
na semantiki zinajishughulisha na maana, kwa hio zipo hisia za ukaribu mno
katika taaluma hizi mbili, licha kwamba pia zipo hisia za karibu za kuonesha
utofauti wao.
Niukweli usiopingika kwamba
kuna maarifa ya lugha na wakati huohuo kuna maarifa ya ulimwengu halisi, hii
inamaana kuwa kufahamu lugha peke yake haitoshi lazima lugha hiyo itumike
kulingana na muktadha au ulimwengu halisi ambapo lugha hio imetumika. Hali hii
inaweza kuthibitishwa kutokana na kuwepo kwa matumizi ya maana tofauti kwa
kadri ya watumiaji husika kama ifuatavyo.
Matumizi
ya maana ya msingi katika kufafanua maana. Hii ndiyo njia kuu ya kulipa neno
maana, ambayo kwa kawaida haibadiliki
kutegemeana na athari za kimazingira. Hii inamaana kuwa maana ya neno au tungo
itabaki ile ile hata kama mazingira yatabadilika. Maaaana hii ndiyo inayojulikana
kama maana ya kileksika. Kwa mfano; kichwa- kikimaanisha sehemu muhimu katika
mwili wa binaadamu kinachokusanya viungo kama vile; macho, masikio, pua na
mdomo. Hii ndiyo maana pekeyake inayohitaji ulimwengu wa lugha kwa kiwango
kidogo sana, hata hivyo bado ulimwengu halisi utahitajika kutokana na matumizi
ya maneno kama vile homophoni na homonimia. Mfano neno kama kaa licha ya
kuwepo kwa maarifa ya lugha lakini bado
maarifa yaulimwengu halisi yanahitajika kuelewa kusudio la mzungumzaji, kwani
yapo mazingira ambayo neno hilo litaendelea kutumika kama kitendo cha kuketi,
na mazingira mengine litumike kama cheche la moto, na yote hayo ni maana ya
msingi ya neno kulingana na miktadha tofauti tofauti.
Maana ya
ziada au kisarufi. Ni maana abayo huibuka kutokana na maana ya msingi. Maana hii
inatudhihirishia kuwepo kwa maarifa ya lugha na wakati huohuo kuna maarifa ya
ulimwengu halisi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, maana hizi hutegemeana na
kuhusiana na mazingira halisi ya matumizi. Kuelewa maana ya ziada sio tu
kuelewa maarifa ya lugha, bali pia ulimwengu halisi au muktadha ambapo maneno
au fahiwa hizo zimetumika. Mfano pale mzungumzajia atakapo sema “Samahani kaka!
Hivi utaendelea kuwa kupe hadi lini? haya ni maisha tu!” utagundua kuwa, hapa
kufahamu maana ya tungo hii si kutokana tu na kufahamu maarifa ya lugha, lakini
pia inahitajika ufahamu wa ulimwengu halisi ambao tungo hio imetumika, kwa
kusema kupe kumaaanisha mtu mnyonyaji au mtegemezi.
Maana ya kimtindo. Hii ni maana inayohusiana moja
kwa moja na matumizi ya lugha kulingana na muktadha husika. Katika aina hii ya
maana, neno au kiyambo hupata maana kulingana na mtindo ambao neno au kiyambo
hicho kimetumika. Mfano mtindo wa kilahaja, mtindo wa wakati, mtindo wa kieneo,
au hata mtindo wa taaluma ua fani fulani. Ni lazima tukiri kwamba kuna marifa
ya lugha lakini wakati huo huo kuna ulimwengu halisi. Hii ni kwa maana kwamba
katika maana hii, lazima mtumiaji wa lugha licha ya kufahamu maarifa ya lugha
hio, lakini lazima azingatie ulimwengu halisi ambao lugha hio imetumika. Mfano matumizi
ya mtindo wa kilahaja, kuna baadhi ya maneno kiuhalisia huibua hisia zingine na
wakati mwingine kushindwa kufahamika kutokana na tofauti za kilahaja. Mfano
maneno kama vile, shule, ugali na bomba, maneno haya yanaweza kutumika katika
hali tofauti kwa wakaazi wa Tanzania bara na visiwa vya Zanzibar. Kwa upande wa
Zanzibar wangeweza kutumia skuli, sembe na mfereji kwa mfuatano. Hivyo basi,
kwa mzungumzaji inampasa kujua ni akina nani anazungumza nao na nani wangeweza
kumuelewa ingawa wate wana maarifa ya lugha moja.
Aidha, kuwepo kwa maana hisia ni ithibati tosha
ya kuthibitisha kuwepo kwa maarifa ya lugha na wakati huohuo ulimwengu halisi katika
dhana ya semantiki na pragmatiki zinazohusu maana. Tunapozungumzia maana ya hisia ni aina ya maana ambayo huibuka
kutokana na hisia au mtazamo wa msemaji au mwandishi. Na maana hii huweza
kuwasilishwa kwa njia mbalimabali zikiwemo, njia ya maana kama dokezi au njia
isiyo ya moja kwa moja. Kwa mfano “kweli wewe ni kidume wa mbegu kwelikweli!” katika
tungo hii ni vigumu kufahamu mzungumzaji amemaanisha nini ikiwa msikilizaji
hatohusisha maana au kauli hii na ulimwengu halisi au muktadha ambao msemaji au
mwandishi amezungumza au kukusudia, kwani maana ya msemaji itakua tofauti na
maana ya msikilizaji atakayojengwa kwa kuzingatia tu maarifa ya lugha.
Mathalani hapa tunaweza kusema kuwa, msemaji amekusudia huyu kijana ni mchapakazi
kwelikweli. Au kwa waswahili wanakawaida ya kumsifia mtu kwa kusema kwa mfamo,
huyu mchezaji yaani hafai, mshenzi kwelikweli! Kiuhalisia neno hafai
linamaanisha hali hasi ya mtu, vile vile mshenzi ni neno linalotaswira mbaya ya
ufedheheshaji, lakini waswahili husema hivyo kuonesha sifa njema za mtu,
tofauti n auhalisia. Hivyo kwa mtu kufasiri maana kulingana na maarifa ya lugha
inapelekea kupotosha maana iliyokusudiwa.
Maana tangamani. Hii ni maana inayopatikana
kutokana na matumizi ya lugha kulingana na muktadha husika wa matumizi kwa
kuzingatia maana ya maneno mbalimbali na jinsi yanavyotumiwa kwa pamoja ili
kuleta maana iliyokusudiwa. Maana hii pia inatuthibitishia kuwepo kwa maariufa
ya lugha na wakati huohuo ulimwengu halisi. Hii inamana kuwa si kujua tu
maariufa ya lugha ndio kuweza kuitumia lugha hio, lakini ni kwa vipi lugha hio
ingeweza kutumika. Kwa mfano kauli kama vile “Mabibi na mabwana”, mvulan
amtanashati, dada mrembo. Ukichunguza tungo hizi utagundua kuwa si kufahamu tu maarifa
ya lugha, bali lazima mtumiaji afahamu ulimwengu halkisi wa matumizi ya maneno
hayo. Mfano msemaji angeweza kusema, ‘mabibi na mababu” au “dada mtanashati” na
‘mvulana mrembo” jambo ambalo lisengekubalika kajika jamii za waswahili.
Maana mangwi au akise. Ni aina ya maana ambayo
huibuka katika hali ambayo maana moja hukonyeza maana nyingine na hivyo
humfanya mtu afikirie maana nyingine pia. Mfano kauli “naenda kujisaidia” Katik
tungo hii inahitaji mtumiaji wa lugha au msikilizaji kufahamu ulimwengu halisi,
yaani wanajamii fulani wanavyosema kujisaidia
wanamaanisha nini? Kwa mfano mara nyingio katika jamii za kiafrika kujisaidia
humaanisha ima kuenda haja ndogo au kubwa. Jambo hili katu lisengefahamika kwa
sababu tu ya kufahamu maariga ya lugha hio.
Mwisho ni maana ya dhamira au muhimu. Hii ni
aina ya maana ambayo hutegemea kile ambacho mtoa ujumbe ana kipa umuhimu zaidi.
Mara nyingi kile kinachopewa umuhimu zaidi hutokeza mwanzoni mwa senmtensi.
Msingi wa kupata maana katika aina hii inathibitisha kuwa pamoja na kuwa na
marifa ya lugha pia panakuwepo n aulimwengui halisi wa lugha. Kupitia aina hii
ni vigumu mtu kutambua umuhimu wa msemaji au mzungumzaji kwa msingi tu wa maarifa
ya lugha bila kuhusisha hali gani lugha hio imetimika. Mfano kauli ya kusema
“Kikwete atashinda uchaguzi wa mwaka 2015” Katika mfano huu umuhimu zaidi upo
kwa Kikwete ndiye ambaye ana tarajiwa kushindsa uchaguzi na sio uchaguzi wala
mwaka 2015. Haya yote yatabainika ikiwa tu msikilizaji atakuwa anamaarifa ya
lugha na wakati huohuo anaujua ulimwegu halisi.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, semantiki na pragmatiki zote kwa pamoja
zinahusiana, kwa mana kwamba zinajihusisha na maana ya maana katika lugha. Wala
haitokuwa sahihi kudhani kwamba kufahamu tu maana ya viambajengo katika tungo,
iwe neno, kirai, kishazi au hata sentensi kuwa ndio kufahamu kwa kile kilichokusudiwa
bila kujali muktadha ambao neno hilo
imetumika.
Hat hivyo, taaluma hizi bado
zitaendelea kuwa tofauti kwa kuwa semantiki hujihusisha na maana za maneno au
viyambo vya maneno kama vilivyo kupitia kwa masemaji na msikilizaji. Wakati
huohuo pragmatiki hujishughulisha na jinsi
gani muktadha unapelekea kupata maana ya kile kilichokusudiwa kulingana na muda
mahsusi.
Aidha ifahamike kuwa Semantiki na Pragmatiki zote kwa pamoja
zimelenga kutoa ufafanuzi kuhusu mchakato
wa lugha na matumizi yake kulingana na muktadha wa uzungumzaji au utumikaji
wake. Kama sehemu ya mfumo wa mazungumzo , sambamba na kufasiri na kufafanua
mfumo fungamanifu wa mazungumzo katika
lugha, na hili litafikiwa tu kwa kuzingatia maarifa ya lugha sambamba na
ulimwengu halisi wa mazungumzo.
MAREJEO.
Geoffrey Finch,
(2000).
Linguistic Terms and Concepts. Palgrave Macmillan.
Jacob L. Mey, (2001). Pragmatics: An Introduction, 2nd ed. Wiley-Blackwell.
Richmond
H Thomason (2012). What is semantics? Second version.
Wwww.wisegeek.com Publishing & Printing International Journal. (USA),
downloaded on Friday, 30th May 2014, at 12:30 pm.
Yule, G. (1996). Pragmatics. Oxford: Oxford University
Press.
Kazi nzuri.
ReplyDeleteTafadhali jadili mahusiano ya isimu kwa kijumla na taalima nyingine kama Historia, Anthropolojia na saikolojia.
ReplyDeleteSafi sana imenisaidia
ReplyDeletenzuri hiyo
ReplyDeleteKAZI NZURI SANA
ReplyDeleteAllah akubariki
ReplyDeleteUmeeleza vzr sana jaribu kufafanua kwa maw and a take mapana
ReplyDeleteNitmumie kwa email yangu
ReplyDelete