Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ametoa dira ya
urais katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kutaja sifa za rais anayefaa kuiongoza
Tanzania.
Warioba amesema, taifa la Tanzania linastahili kuongozwa na
vijana wenye nguvu ya mwili na akili.
“Mimi nafikiri tuangalie kati ya vijana tulionao, nani
anatufaa kuiongoza nchi, tusirudi kuangalia wazee,” alisema Jaji Warioba
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya mwandishi wa
habari hizi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika wiki hii ofisini kwake
jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja huku ukiwa umesalia
takribani mwaka mmoja na miezi minne, kabla ya taifa kuingia kwenye
kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaoshirikisha
vyama zaidi ya 23 vyenye usajili wa kudumu nchini.
Uchaguzi huo mkuu ambao ni wa tano wa vyama vingi nchini,
unatarajiwa kulipatia taifa rais mpya, baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza
muda wake wa utawala wa awamu ya nne.
Mbali na wagombea wa vyama vya upinzani, ndani ya CCM pekee kunatajwa kuwa na makundi zaidi ya manne yanayotarajia kuwania urais mwaka ujao.
Makundi hayo ni pamoja na linalotajwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, kundi lingine linatajwa kuwa nyuma ya Samuel Sitta ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na linalomuunga mkono Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu, Stephen
Wassira anatajwa kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini.
Hata hivyo, viongozi hao wamekuwapo madarakani katika
nyadhifa na nyakati tofauti huku pia wakiwa na umri uliovuka ujana, unaopendekezwa
na Jaji Warioba.
Ndani ya CCM vijana wanaotajwa kutaka kuwania urais mwakani
ni pamoja na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Makamba tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais akisema
huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola, licha ya chama hicho kuzuia
kutangaza nia na kupiga kampeni kabla ya muda.
Makamba, mmoja wa makada wa CCM walioonywa na chama hicho
baada ya kutuhumiwa kuanza kampeni mapema, alijipigia debe kuwa iwapo
atapitishwa na chama hicho, ataelekeza nguvu kwenye vipaumbele vinne ambavyo ni
ajira, huduma za jamii, uchumi imara na utawala bora.
Akizungumzia uzoefu Makamba alisema hakuna ushahidi wowote
kwamba miaka mingi kwenye siasa ndiyo inatengeneza kiongozi mzuri.
“Uongozi mzuri unatengenezwa na haiba, wajihi, dhamira,
uwezo, maadili, uhodari, hekima na maarifa. Sifa hizi hazipatikani kutokana na
uzoefu wa miaka mingi kwenye siasa hata baadhi ya vijana wanazo,” alisema
Makamba.
Alitolea mifano mingi duniani ambapo vijana ambao hawakuwa na uzoefu kabisa katika nafasi za siasa wameshinda na kubadilisha nchi kama Tony Blair wakati anakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza aliongoza nchi hiyo kubwa wakati alikuwa hajawahi kuwa hata Naibu Waziri.
“Barack Obama (Rais wa Marekani) alikuwa Seneta miaka mitatu tu, Julius Nyerere alikuwa Mwalimu akaingia siasa akaja kupewa uongozi wa nchi akiwa na miaka 39 tu.”

Hata hivyo, Februari mwaka huu, Kamati Kuu ya CCM iliwapa
onyo kali makada wake sita akiwamo January Makamba ikiwatuhumu kupiga kampeni
za urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao kabla ya muda.
Katika maelezo yake Jaji Warioba amesema kwamba tangu uhuru,
walioshika madaraka ya kuliongoza taifa walikuwa ni vijana
Akijibu swali kama atakuwa tayari wananchi wakimtaka kuwania
urais baada ya kazi kubwa ya kukamilisha Rasimu ya Katiba nchini, Jaji Warioba
alisema:
“Hili nilikwishalijibu, tusahau mawazo kwamba sisi (wazee)
tutarudi madarakani. Nadhani mara ya mwisho tulipozungumza niliwaambia inafika
wakati kiongozi unang’atuka. Unawaachia vijana ambao wana nguvu ya kimwili na
akili ndiyo watumikie taifa hili, waongoze nchi.
“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.
“Na mimi nashangaa kwa nini, kwa kweli nashangaa kabisa kutajwatajwa huku, wazee kama mimi na Salim (Dk Salim Ahmed Salim). Nini kimetokea katika nchi hii hata sisi tufikiriwe?” alihoji Jaji Warioba.
Amesema kuwa tangu uhuru hadi sasa Tanzania imetayarisha
vijana wengi wanaofaa kuliongoza taifa na kuongeza:
“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”
“Hatuna ombwe la uongozi, tunao vijana wengi sana, tena kwa bahati nzuri nchi kwa kiwango kikubwa ilikuwa ikiongozwa na vijana.”
Huku akitaja mifano ya viongozi hao vijana walioongoza taifa,
Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema:
“Tulipoanza Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi wa nchi hii,
alikuwa kijana. Alikuwa hajafika hata miaka 40, hata wenzake walikuwa vijana.
Vijana ambao hawakuwa na uzoefu wa kuendesha Serikali, waliichukua nchi.”
Mwanasheria huyo mkongwe aliyelitumikia taifa katika
nyadhifa mbalimbali ameeleza kuwa hata waliofuata katika kulitumikia taifa
walikuwa vijana.
“…Waliofuata, walioshika nafasi za kuitumikia nchi hii
tuliwaona, walikuwa vijana. Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu), aliingia
akiwa bado kijana, akastaafu bado kijana, bahati mbaya akafariki akiwa pia bado
kijana. Dk Salim aliingia na miaka 42, mimi nilikuwa na 45, Sumaye aliingia
bado akiwa kijana,” amesema Jaji mstaafu Warioba huku akihoji tena: “Hivi
kimetokea nini sasa tunaanza kuangalia wazee…, nini kimetokea nchi hii tuanze
kufikiria wazee?”
Jaji Warioba alipoulizwa kati ya vijana walio kwenye
uongozi, yupi atafaa kuongoza taifa alisema:
“Sitaki, sitaki majina, … ni sifa. Sifa zipo, hebu mchukue
alizotaja Mwalimu Nyerere mwaka 1995. Tunataka kiongozi mwenye maadili, mwenye
‘commitment’ (kuwajibika),ambaye atasimamia, ataapa kuisimamia Katiba.”
Warioba pia aliulizwa iwapo makundi yanayotajwa kusaka urais
katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kuwa huenda yanahusika na kusuasua kwa
Mchakato wa Katiba Mpya.
Amesema kwamba, yeye na wenzake waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kutafakari mchakato huo unavyokwenda ukihusisha maeneo na makundi mbalimbali.

“Tulikwenda kutafakari, hatutaki kwenda kwenye matukio, wala
kuzungumzia makundi, nasema wote wakae pamoja waone masilahi ya taifa, kwa
sababu wasipokaa pamoja kuna hatari ya mchakato huu wa Katiba Mpya kukwama. Na
kukwama siyo kwa masilahi ya taifa,”alisema.
Ikiwa Rasimu ya Katiba Mpya itapitishwa na mapendekezo yake
ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu, kutalazimika kuwapo kwa Rais wa
Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo
nguvu na mfumo wa kisiasa kubadilika.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment