Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa ramadhan, waislamu nchini Tanzania wametakiwa kufanya tathmini ikiwa wameweza kulifikia lengo la kufaradhishwa kwa ibada hiyo tukufu ambalo ni kuwa wachamungu.
Wito
huo umetolewa na Hajjat mama Raya wakati akizungumza na Radio Kheri ya jijini Dar
es Salaam mapema hii leo.
Mama
Raya amesema miongoni mwa alama za kufikiwa kwa lengo hilo ni pamoja na kutathmini
mafunzo yanayoambatana na Mwezi mtukufu wa ramadhani.
Akitaja
mafunzo hayo amesema, ramadhani ni umoja, upendo, mshikamano, huruma na mapenzi
baina ya waislamu wenyewe sambamba na mafungamano yao na jamii inayowazunguka.
Amesema
lazima kila muislamu ajifanyie tathimini ikiwa mafundisho hayo yameleta athari
katika nafsi yake au laa, huku akizidisha kujipendekeza kwa mola mlezi.
Ikumbukwe
kuwa Hajjat Mama Raya amekuwa msitari wa mbele katika jitihada mbalimbali za
kutoa elimu na mafundisho sahihi ya dini ya kiislamu ndani na nje ya Tanzania.
MUBARAKA
No comments:
Post a Comment