Thursday, July 17, 2014

WAHADHIRI WANASIHIWA KUFUATA MWENDO WA MTUME (SAW)




Wahadhiri na walinganiaji wa dini ya kiislamu nchi Tanzania wametakiwa kufuata utaratibu aliouasisi Mtume Muhammad (SAW) katika kufikisha nasaha kwa waumini wao.


Wito huo uemtolewa na Mwalimu wa Azhari shariif tawi la Tanzania, Samahatu Sheikh Abudul-Salaam Mohammed Abdul-Salaam wakati akizungumza na Radio Kheri jijini dare s Salaam

Sheikh Abdul-Salaam amesema mawaidha mazuri ndio njia pekee bora ya kukibadilisha kizazi kimuelekeo na mwenendo mzima wa mwanadamu huyo.

Amesema, kazi ya daawa imekabiliwa na changamoto kubwa kutokana na kuepo kwa baadhi ya wahadhiri ambao wanakwenda kinyume na mafundisho ya mbora wa manabii, Mtume Muhammad (SAW).

Aidha, Sheikh abdul-Salaam amesema, ili ulinganiaji uweze kuleta tija katika jamii unahitaji misingi imara iliyofundisha katika uislamu.

Akiitaja misingi hiyo amesema  ni pamoja na kulingania kwa hekma, mawaidha mema, na majadiliano yaliyomazuri, ambayo yameepukikana na chuki, dharau, kebehi na huku ikijengwa katika msingi mkuu na imara wa kumcha Allah (SW).

No comments:

Post a Comment