Mkuu
wa Jumuiya ya Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa kusameheana na
kukomeshwa mapigano, ndiyo njia pekee ya kuikwamua nchi hiyo katika hali ya
machafuko inayoendelea nchini humo.
Akizungumza
na vyombo vya habari, Sheikh Oumar Kobine Layama amezitaka pande zinazopigana
nchini humo kukomesha mapigano hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh
Oumar Kobine amesisitiza kwamba kusameheana na kukomeshwa mapigano ndiyo njia
pekee itakayoweza kuinusuru nchi hiyo na machafuko yanayoendelea.
Mkuu
wa Jumuiya ya Waislamu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, mwezi mtukufu
wa Ramadhani ni mwezi wa amani, kusameheana, udugu, umoja, mshikamano na wa
kutakiana kheri baina ya waumini wa dini tofauti.
Matamshi
ya Sheikh Oumar Kobine Layama yanatolewa katika hali ambayo kuna wasiwasi wa
kujitokeza mashambulio
ya wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka dhidi ya
Waislamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Ikumbukwe
kuwa Jumapili iliyopita, Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliungana na
wenzao duniani, kufunga saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment