Israel imetangaza kuthibitisha kwamba vijana wake watatu waliokuwa wamepotea wamepatikana wakiwa wamekufa.
Miili yao imekutwa
katika mji wa Halhul kwenye ukanda wa Gaza, na naibu waziri wa ulinzi wa Israel
Danny Danon amesema kundi la Hamas ndilo lililowauwa vijana hao.
Waziri huyo ametoa
wito wa kuangamizwa kundi hilo, na waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesisitiza
kwamba Hamas itawajibika kwa uhalifu huo ambao inadaiwa kuufanya.
Awali Hamas
ilikataa kukiri wala kukanusha kuhusika na utekaji nyara wa vijana hao.
Radio ya
serikali ya Israel imesema miili ya vijana hao ilikuwa imefunikwa kwa vipande
vya miamba karibu na mahli walipoonekana mara ya mwisho, kaskazini mwa mji wa
Hebron.
Hata hivyo,
imeelezwa kuwa mpaka sasa bado mazingira ya kifo chao hayajabainika.
No comments:
Post a Comment