Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa,
watu 173 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya utawala haramu wa Israel
katika eneo la Ukanda wa Gaza huku wengine 1, 200 wakijeruhiwa.
Idadi hiyo imeongezeka kufuatia watu saba kuuawa
shahidi hapo jana akiwemo mtoto mchanga huku kijana mwingine akiuawa katika
shambulizi la anga katika eneo la Rafah.
Wakati huo huo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya
Palestina, Mahmoud Abbas ameutaka Umoja wa Mataifa kuwasaidia Wapalestina.
Abbasi ametoa ombi hilo kupitia barua
aliyoiwasilisha kwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina
zinazokaliwa kwa mabavu, Robert Serry akimtaka awasilishe ujumbe huo kwa Katibu
Mkuu wa umoja huo.
Abbasi amesema kuwa, serikali ya Palestina
imekwishachukua maamuzi maalumu ambayo yatatangazwa hivi karibuni kuhusiana na
mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.
No comments:
Post a Comment