Jaji Mkuu wa Kenya, Willie Mutunga, amewataka
majaji wanaosikiza kesi zinazohusiana na ugaidi kuwa wabunifu katika maamuzi
yao ili kulinda maslahi ya taifa.
Mutunga amesema imekuwa vigumu kushinda vita
dhidi ya ugaidi kutokana na baadhi ya majaji kupuuza kilio cha walio wengi na
usalama wa taifa na badala yake wamekuwa wakijifunga zaidi kwenye tafsiri za
kisheria.
Jaji Mkuu wa Kenya amesema majaji wanapaswa
kuweka kwenye mizani haki na maslahi ya taifa ili kufikia maamuzi yenye busara.
Amekumbusha kuwa, mahakama kama moja ya
mihimili mitatu ya dola inawajibu wa kulinda maslahi ya taifa sambamba na kutoa
haki kwa washukiwa.
Mahakama za Kenya zimekuwa zikilaumiwa kwa
kuwaachilia huru kwa dhamana baadhi ya washukiwa wa ugaidi jambo linalozidi
kuwapa nguvu magaidi na wahalifu wengine.
No comments:
Post a Comment