Bunge
maalumu la katiba linatarajiwa kuanza leo njini Dodoma ikiwa ni sehemu ya pili
baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia kupisha Bunge la Bajeti ya Serikali.
Wakati
watanzania wakisubiri kwa hamu juu ya mustakbali wa mchakato wa katiba mpya,
wananchi, wadau, na taasisi mbalimbali za dini na za kiserikali zimekuwa na
mitazamo tofauti tofauti hasa kutokana na mwenendo wa mchakato huo.
Wakizungumza
na Radio Kheri kwa nyakati tofauti na katika mikutano ya wazi na ya siri, wadau hao kutoka bara na visiwani, wameendelea
kuliombea bunge hilo, huku wakiwasihi wajumbe hao kuangalia zaidi mustakbali wa
taifa badala ya kuangalia maslahi ya makundi yao.
Kwa upande
wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka wajumbe wa bunge hilo
kuacha malumbano badala yake wajadili rasimu ya katiba ambayo mwisho wake
itakuwa ni kupigiwa kura na wananchi.
Nae
Mwenyekiti wa wa kamati iliyoundwa na wananchi waliohudhuria midahalo ya wazi
kuhusu mchakato wa katiba mpya iliyoandaliwa na Taasisi ya utafiti na sera za Umma
Zanzibar(ZIRPP), Bwana Ali Abdulla Salum amemuomba Raisi Kikwete akishirikiana
na Drt. Shein kutumia hekima kuunusuru mchakato huo, kwani kama katiba mpya
itakosekana Tanzania itaingia katika giza la kisiasa.
No comments:
Post a Comment