Rais
Jakaya Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya Nyota wa Demokrasia
Afrika kwa mwaka huu.
Kwa
mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar es Salaam,
Rais Kikwete, amekuwa mshindi wa kwanza na kuwaacha wenzake mbali katika
mchuano na marais watatu wa Afrika ambao walifikia mwisho mchuano wa kuwania
tuzo hiyo.
Katika
barua iliyochapishwa na Mchapishaji na Mhariri Mkuu wa Jarida la The
Voice, Pastor Elvis Iruh, akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Tuzo 2014, amesema
uongozi wa Rais Kikwete umekuwa ni hadithi ya kusifiwa ya mafanikio katika Bara
la Afrika ambako hadithi za namna hiyo siyo nyingi.
Tuzo
hiyo hutolewa na Jarida la The Voice na mwaka jana mshindi alikuwa ni Rais Bai
Koroma wa Sierra Leone ambaye alikuwa ni mshindi wa pili wa tuzo hiyo, iliyotolewa
kwa mara ya kwanza kwa Rais wa Kwanza wa Zambia, Mzee Kenneth Kaunda.
Miongoni
mwa sifa zilizopelekea Rais Kikwete kutunukiwa tuzo hiyo ni kuwa msimamizi
mzuri wa demokrasia, kuendelea kuhakikisha kuwa amani, utulivu na maendeleo vinaendelea
kupatikana katika eneo la Afrika ambalo limepitia vipindi vingi vya migogoro na
matatizo.
No comments:
Post a Comment