Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Tanzania na
Malawi zinasubiri kuitwa kwenda Maputo nchini Msumbiji kwa ajili ya kuendelea
na hatua nyingine ya usuluhishi wa mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya
pande mbili hizo.
Waziri
Membe amesema hayoa katika ujumbe wake mfupi kwa waandishi wa habari uliolenga kujua ratiba ya usuluhishi huo kwa sasa baada
ya Malawi kumaliza uchaguzi mkuu wake Mei mwaka huu.
Ameongeza kuwa “Makubaliano ya mwezi Machi,
mwaka huu, yalikuwa ni kuwataka wazee hao kuitisha kikao mara baada ya Malawi kumaliza
uchaguzi wake
Mchakato
wa kuendelea na usuluhishi wa mgogoro huo, ulisitishwa kwa muda baada ya
Serikali ya Malawi kuliomba jopo la usuluhishi, lisubiri kumalizika kwa
uchaguzi mkuu nchini humo ambao ulifanyika Mei mwaka huu.
Mgogoro
wa mpaka wa Ziwa Nyasa uliibuliwa na aliyekuwa Rais wa Malawi, Joyce Julai
mwaka juzi, kwa madai ya kwamba, eneo lote la ziwa hilo lipo upande wa nchi
hiyo kinyume cha sheria za kimataifa zinazotaka kila upande kumiliki sehemu ya
maji kwa asilimia 50 kama ilivyokuwa kabla ya hapo kwa miaka mingi.
No comments:
Post a Comment