Jiji la Arusha limekumbwa na taharuki baada ya
kuibuka kwa matukio ya wanawake wanaoendesha magari kuvamiwa na kupigwa risasi
na watu wasiofahamika ambao hutoweka bila kuchukua chochote.
Vyanzo vya habari mjini humo vimeeleza kuwa, hadi
sasa, wanawake watatu wamekumbwa na kadhia hiyo huku mmoja akifariki.
Aidha, Jeshi la Polisi linaangalia uwezekano wa
kufunga kamera ili kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayolikumba Jiji, na kwa
sasa wanaendelea na majadiliano na wadau mbalimbali ili kufanikisha hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas,
jamethibitisha kutokea kwa matukio hayo, ambayo amesema kuwa mawili yametokea
eneo la Sakina kwa Iddi na moja Mbauda.
Amesema hadi sasa hawajajua sababu ya matukio
hayo, ambayo walengwa wakuu wamekuwa ni wanawake wanaoendesha magari, hivyo kuiomba
jamii kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu hao.
Sabas, amemtaja aliyefariki kuwa ni Shamim
Yulu, (30), ambaye alipigwa risasi shingoni juzi majira ya saa 3.30
usiku wakati akikaribia kufika kwenye lango la nyumba yake maeneo ya Sakina kwa
Iddi.
No comments:
Post a Comment