Wednesday, August 27, 2014

WAHITIMU VYUO VIKUU JIUNGENI UJASIRIAMALI



DAR ES SALAAM

Wahitimu wa vyuo vikuu nchini wameshauriwa kujiunga na ujasiriamali badala ya kuzunguka  na vyeti kutafuta ajira ambazo ni chache.


Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Dina Bina, Mkurugenzi wa kampuni ya Dinaflowers katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Chuo Kikuu cha Uingereza kwa wanafunzi wajasiriamali wa vyuo vikuu vya  Tanzania.


Bina amesema vijana wengi wamejijengea mazaoe mabaya kuwa wakimaliza Chuo Kikuu hawawezi kuuza nyanya na bidhaa nyingine mpaka apate kazi ofisini, kitu ambacho kinapelekea vijana wengi kukaa nyumbani kwa miaka zaidi ya mitano wakisubiri ajira wakati umri wao unakwenda.


Amesema vijana wanatakiwa kuiga mfano wa baadhi ya wafanyabiashara nchini kutokana na walivyofanikiwa.


Msuva Ocheki, Mkurugenzi wa Cmbridge Devolopment Initiative upande wa Tanzania amesema wameanza kuhakikisha vijana wengi wanaondokana na mawazo ya kuajiriwa badala yake wajifunze kujiajiri wenyewe.

No comments:

Post a Comment