Wednesday, August 27, 2014

KATIBA MPYA ITAMKE UMRI WA NDOA MIAKA 18



DAR ES SALAAM

Watanzania wameaswa kukitumia kipindi hiki cha kuundwa kwa Katiba mpya kuwa na kifungu kwenye katiba kinachoeleza umri wa ndoa kuwa miaka 18 na kuendelea, ili kuondoa tatizo la ndoa za utotoni.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Grace Machel, alipokuwa akizundua kampeni ya kitaifa dhidi ya ndoa za utotoni inayoanzia katika wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.

Machel amesema ni muhimu kwa wadau wote wa haki za watoto wakashinikiza wajumbe wa Bunge Maalumu na watunga sheria wote wahakikishe kipengele hicho kinaingia ndani ya katiba.

Amesema ni juu ya wadau wote serikalini, asasi zisizo za kiserikali, taasisi za kidini na wananchi wenye mapenzi mema kuyaelimisha makundi haya yakubali uwepo wa sheria ndani ya katiba inayotamka kuwa mtoto ni mwenye umri chini ya miaka 18.

Naye, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, pamoja na kuunga mkono kampeni hiyo, ametoa wito kwa watoto kujitokeza hadharani na kutumia fursa zote wanazozipata kupaza sauti dhidi ya mbinyo wa haki zao, likiwamo suala la ndoa za utotoni.



No comments:

Post a Comment