Mahakama nchini Misri
imemhukumu kiongozi wa kidini wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohamed Badie
kifungo cha maisha jela, yeye pamoja na wafuasi wake wapatao kumi na wanne.
Badie ameshitakiwa kwa kosa la mauaji na
kuchochea ghasia katika eneo la Giza mwaka 2013.
Tayari anatumikia kifungo cha maisha baada ya
kupatikana na hatia ya kuchochea ghasia za kupinga kuondolewa madarakani kwa
aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.
Awali alipewa hukumu ya kifo ambayo ilipunguzwa
na kufanywa kifungo cha maisha mwezi Agosti.
Bwana Badie peke yake anakabiliwa zaidi ya kesi
30 kwa kuchochea ghasia.
Hata hivyo mwanaharakati mashuhuri Alaa
Abdel-Fattah, ameachiliwa huru katika mahakama nyingine.
Alaa alihukumiwa miaka 15 jela kwa kushiriki
katika maandamano ambayo yalizuiwa mnamo mwaka wa jana.
No comments:
Post a Comment