Ubalozi wa Assia nchini Tanzania umeandaa
tamasha maalumu litakaloonesha filamu ya hali ya taifa la Wapalestina na jinsi
linavyokandamizwa na utawala ghadhibu wa Israil.
Tamasha hilo litakuwa ni la 9 kufanyika, ambapo
mwaka huu litaanza Octoba 17 hadi 27,
likitambulisha filamu ijulikanayo kama “Omar” na kufasiriwa kwa lugha ya Oman.
Hayo yamesemwa na Dr Nasri Abujaishi katika mkutano maalumu na waandishi wa habari
uliofanyika katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam mapema hii
leo.
Mkutano huo pia umeweza kuhudhuriwa na mabalozi
kutoka nchi mbali mbali zikiwemo, China, india, Indonessia, Iran, Pakistani,
Oman, South Korea, japan, Vietnam, UAE, na Palestina.
Dr Abujaishi amasema kuwa lengo na dhumuni la
kuandaa filam hiyo nikutaka kuufahamisha ulimwengu juu ya kadhia ya Israil na
mustakbali wa Taifa la wapalestina kama taifa huru.
Kwa mujibu wa Dr Abujaishi ukandamizwaji wa
wapalestina dhidi ya utawala ghadhibu wa Israel
umeanza tokea waislrail walipovamia baadhi ya vijijni na miji ya
wapalestina miaka ya 1948.
No comments:
Post a Comment