Makamo
wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar, Maalim Seiff Shariff Hamad amesema
haikubali Katiba inayopendekezwa kwa kuwa haina maslahi ya wazanzibari
na badala yake atawashawishi kuipigia kura ya hapana.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya
Demokrasia vya Kibanda Maiti, mjini Zanzibar ukiwa ni Mkutano wa kwanza mkubwa
tokea kumalizika kwa mchakato wa katiba mpya inayopendekezwa.
Amesema
kuwa miongoni mwa mambo yanayoipokonya Zanzibar hadhi yake ni Katiba
inayopendekezwa kumpokonya Rais wa Zanzibar mamlaka ya kugawa mikoa, tofauti na
Katiba ya Zanzibar ya sasa.
Amesema
kwa maana hiyo Rais wa Muungano anachukua mamlaka ya Rais wa Zanzibar na
anaweza kuteua wakuu wa mikoa, na wakuu wa wilaya wa Zanzibar.
Amesema
hakubaliani na kauli za baadhi ya watu wanaosema kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inaridhishwa na mchakato wa Katiba mpya.
No comments:
Post a Comment