Maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa asilimia 90.
Hayo yamesemwa na Meneja wa shirika la EGPAF
Mkoa wa Tabora, Dk. Alphaxard Lwitakubi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete
kukagua banda la shirika hilo katika maonyesho ya wiki ya vijana.
Lwitakubi, amesema lengo la EGPAF ni kufikia
asilimia 98 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015.
Amesema hatua hiyo itafikiwa endapo wanaume
wataambatana na wake zao kwenda kwenye vituo vya afya kama inavyotakiwa, kwani
hadi sasa zimefikiwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 5 mwaka 2010.
Dk. Lwitakubi, amesema Shirika la EGPAF
limekuwa likijihusisha na kazi za kuzuia na kutokomeza maambukizi ya virusi vya
Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mawasiliano na Utetezi
wa EGPAF, Mercy Nyanda, amesema katika huduma zao kumekuwa na mafanikio, kwani
kwa sasa wajawazito wengi wanajifungulia vituoni tofauti hapo mwanzo.
No comments:
Post a Comment