Serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi
bilioni 18 kwa ajili ya chanjo ya surua na ribela inayotarajiwa kutolewa Oktoba
18 mwaka huu nchini kote.
Hayo yamesemwa na Ofisa mafunzo na mawasiliano
wa idara ya kinga na chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Ibrahim
Maduhu wakati wa mkutano wa kamati ya huduma ya afya ya msingi wa jiji la
Tanga.
Amesema kuwa uwekezaji huo ni mkubwa kufanywa
na serikali kwa wananchi wake kwa lengo la kuwapatia afya bora.
Dk Maduhu amesema, kuwa ni jukumu la kamati za
afya nchini nzima
kuhakikisha wanaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo.
kuhakikisha wanaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo.
Naye mganga mkuu wa jiji hilo, Dk Asha Mahita
amesema, kuwa asilimia 15 ya watoto waliopatiwa chanjo ya surua katika jiji
hilo hawajajenga kinga kamili.
No comments:
Post a Comment