Jamii za wafugaji zinadaiwa kukabiliwa na
kiwango kikubwa cha tatizo la kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
unaochangiwa na wajawazito kukosa vitamini itokanayo na mboga za majani
kutokana na kitoweo chao kikubwa kuwa nyama.
Katika hatua nyingine imeshauriwa miezi miwili
au mitatu kabla ya kubeba ujauzito, mwanamke awe amepata vitamini aina ya
follic acid ama kupitia ulaji wa mboga na matunda au kwa kupata vidonge maalumu
kwa ajili ya kukabili tatizo hilo.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha
Wazazi wa Watoto wenye Matatizo ya Mgongo Wazi na Kichwa Kikubwa (ASBAHT),
Abdulhakim Bayakub katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
jijini Dar es Salaam.
Bayakub pamoja na tatizo hilo, amezungumzia
Maadhimisho ya Siku ya kupunguza uzao wa watoto wenye ulemavu huo amesema yatafanyika
Oktoba 25 katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) jijini Dar es Salaam.
Amesema watoto wengi wamekuwa wakicheleweshwa
kufikishwa hospitalini kutokana na sababu mbalimbali miongoni mwake ikiwa ni
imani za kishirikina wakiamini kwamba tatizo hilo limetokana na uchawi.
No comments:
Post a Comment