Tuesday, September 16, 2014

MOHAMMED BADIE AISHIA KIFUNGO CHA MAISHA





Mahakama nchini Misri imemhukumu kiongozi wa kidini wa kundi la Muslim Brotherhood, Mohamed Badie kifungo cha maisha jela, yeye pamoja na wafuasi wake wapatao kumi na wanne.

Badie ameshitakiwa kwa kosa la mauaji na kuchochea ghasia katika eneo la Giza mwaka 2013.

Tayari anatumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kuchochea ghasia za kupinga kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.

Awali alipewa hukumu ya kifo ambayo ilipunguzwa na kufanywa kifungo cha maisha mwezi Agosti.
Bwana Badie peke yake anakabiliwa zaidi ya kesi 30 kwa kuchochea ghasia. 

Hata hivyo mwanaharakati mashuhuri Alaa Abdel-Fattah, ameachiliwa huru katika mahakama nyingine.
Alaa alihukumiwa miaka 15 jela kwa kushiriki katika maandamano ambayo yalizuiwa mnamo mwaka wa jana.

No comments:

Post a Comment