Takriban
watu 48 wameuwawa kwa risasi kwenye mji wa Mpeketoni uliopo karibu na kisiwa
cha Lamu nchini Kenya.
Polisi
nchini humo imesema kuwa watu wanne waliokuwa na silaha waliteka magari mawili
na kuyaamrisha kuelekea eneo la Mpeketoni ambapo walianza kuwafyatulia watu
risasi kiholela.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema, kundi moja lilishambulia mikahawa , kituo cha polisi
pamoja na kituo cha mafuta kwa saa kadhaa.
Haikuchukua
muda mrefu, miili ilionekana kutapakaa kila mahala huku maeneo mengine
yakiteketezwa nkwa risasi za moto.
Mpaka sasa
hakuna mtu yeyote ambaye amesadikiwa kukamatwa na polisi juu ya tukio hilo la
kusikitisha.
Hata hivyo, Polisi wameendelea kulishuku kundi la wanamgambo wa Al
Shabaab kuwa ndio waliotekeleza mauwaji hayo.
Kwa upande wa kundi hilo, bado halijatoa tamko rasmi juu ya
kuhusika au kutohusika na kitendo hicho, au kutokana na polisi kulishuku kundi
hilo kuhusika na mauwaji hayo.
No comments:
Post a Comment