Mahakama nchini Sudan imemhukumu mwanamke mmoja adhabu ya
mijeledi 100 baada ya kuthibitika kufanya kitendo kichafu cha zinaa.
Daktari Mariam Yahya
Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muislamu alishitakiwa kwa kosa la zinaa na kasha
kuishi na mwanamme mkristo wakiendeleza
zinaa hiyo kitu ambacho ni kinyume na sheria ya Allah (SW)
Mariam mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni mjamzito pia atapata
adhabu ya mijeledi 100 kwa kosa la zinaa.
Maofisa wakuu wamesema kuwa licha ya Mariam kulelewa kwa njia
ya kikristo yeye bado ni muislamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake na wala hajawaki kuritadi, hivyo lazima sheria
ya kiislamu ichukue mkondo wake.
Kwa kawaida uislamu umeharamisha matendo machafu ya zinaa, na
kuweka adhabu kali kwa yeyote atakaekaribia unyama huo kwani athari yake si
kwake tu bali hata kizazi kitakachofatia.
Hata hivyo, Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu
Amnesty International limekuja juu na kusema kuwa Bi. Ishag alilelewa kama
mkristo muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
No comments:
Post a Comment