Sunday, June 1, 2014
ABUJA Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imesema inachukua hatua imara zaidi za kukabiliana na kundi la Boko Haram nchini Nigeria. Uamuzi huo umetangazwa katika taarifa ya mwisho baada ya kikao cha dharura cha viongozi wa ECOWAS waliokutana mjini Accra Ghana. Aidha kikao hicho kimetangaza kushirikiana na nchi za kati mwa Afrika katika kuliangamiza kundi la Boko Haram. Tangazo hilo la ECOWAS linakuja punde baada ya Nigeria, Chad, Cameroon na Nigeria kutangaza vita dhidi ya Boko Haram. Wakati huohuo , wananchi wa Nigeria wameitaka serikali ya Rais Goodluck Jonathan kutoeneza machafuko katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Ikumbukwe kuwa, wanamgambo wa Boko Haram bado wanawashikilia mateka wasichana wa shule wapatao 223 waliotekwa nyara hivi karibuni katika Jimbo la Borno kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment