Sunday, June 1, 2014

BANGUI Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamuru kuwa makundi yote yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yaweke chini silaha zao. Hayo yamekuja wakati Baraza hilo likilaani wimbi la hivi karibuni la machafuko nchini humo, ikiwa ni pamoja na shambulizi lililofanywa mji mkuu wan chi hiyo Kufuatia shambulizi hilo, watu 17 waliuawa katika tukio hilo na wengine 27 bado hawajulikani waliko. Baraza la Usalama limesema viongozi wa mpito nchini humo wana jukumu la msingi kuwalinda wananchi hivyo hawanabudi kuchukua hatua zinazofaa ili kuzuia machafuko zaidi nchini humo. Kupitia hotuba ya televisheni, rais wa mpito Catherine Samba Panza ameahidi kuwa waliohusika wa shambulizi hilo wataadhibiwa na kuwa makundi yenye silaha mjini Bangui yatapokonywa silaha hizo.

No comments:

Post a Comment