Sunday, June 1, 2014
BANGUI Waislamu wameandamana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, wakitaka wahamishwe kutoka mji huo kutokana na hujuma za kinyama za magaidi wa kundi la Kikristo la anti-Balaka. Waislamu wameandamana siku ya Jumamosi katika mtaa wa PK5 wenye Waislamu wengi mjini Bangui ambao ndio kitovu chao cha mwisho mjini humo. Waandamanaji wamelaani vikali hatua ya serikali kuwapokonya Waislamu wa Bangui silaha katika hali ambayo wanakabiliwa na hujuma za anti-Balaka. Kiongozi wa waandamanaji hao Ousmane Abakar amenukuliwa akisema iwapo Waislamu wa mtaa wa PK5 watapokonya silaha basi watu wote wa Bangui nao wanapaswa kupokonywa silaha. Siku ya Ijumaa rais wa muda wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba-Panza alisema serikali yake itawapokonya silaha Waislamu wa mtaa wa PK5. Kiongozi huyo wa CAR ametoa matamshi hayo wakati ambao magenge ya vijana Wakristo yakiendeleza uvamizi na kuubomoa msikiti mmoja mjini Bangui.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment