UISLAMU NA MAENDELEO YA
KISWAHILI
"MWENDA
MAKUTHURIA".
UWASILISHAJI
MUHTASARI.
Katika
makala haya, mwandishi anakusuadia kueleza mchango wa uislamu katika maendeleo
ya Kiswahili. Hii ni baada ya kusoma kazi mbalimbali za wataalamu tofauti na
kuona kuwa maandiko mengi yanaelezea maendeleo ya Kiswahili yalivyochangiwa na
dini ya kikristo, vita, biashara, utawala wa kikoloni na kusahau mchango
uliotolewa na uislamu.
Mwandishi
anauona mchango uliotolewa na dini ya kikristo kama vile wamishionari walioandika
na kufanya kazi mbalimbali katika kukuza Kiswahili kwa mfano John Krapf
aliyekuwa mwanachama wa Shirika la
Wamishiori (Church Missionary Society)
alisaidia sana katika uandaaji wa kitabu kilichoitwa Outline of the Elements of the Kisuaheli
Language with Special Reference to Kinika Dialect. Askofu Edward Steer A Handbook of the Swahili Language as Spoken
in Zanzibar.
Pamoja
na kufasiri nyimbo mbalimbali pia waliandika kamusi za Kiswahili mfano Fredrik
Johnson alipata nguvu kubwa ya kuandaa kamusi iliyoitwa Standard English-Swahili Dictionary na A standarnd Swahili-English Dictionary, hizi zote zilichapishwa
mwaka 1939 na bado zinatumika mpaka leo.
Huu ulikuwa mchango mkubwa sana katika kukuza Kiswahili Afrika Mashariki. Hapa
Kiswahili kinajadiliwa kama lugha na sio kama fasihi.
Kundi
lingine lililochangia kukua na kuendelea kwa lugha ya Kiswahili ni kundi
la wanaleksikografia. Hawa waliandaa
sarufi ya lugha ya Kiswahili katika maandishi hatimaye kukiwezesha Kiswahili
kufundishwa kama lugha ya pili katika Afrika Mashariki ilihali ni lugha ya
wenyeji.
Lakini
pamoja na mchango huo waandishi hawa wameshindwa kueleza ukweli kwani wanaeleza
ukweli wa mchango wa kikristo na kusahau kovu lililoandikwa na Waswahili katika
historia ya Waswahili kuhusu usafirishaji wa mamilioni ya watumwa kwenda nje,
hivyo wamesahau mchango wa uislamu wakati, uislamu uliingia Afrika Mashariki
mapema kuliko dini ya kikristo yaani hata kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya.
Pia
ni wazi kwamba kwa mara ya kwanza wanazuoni wa kiislamu ndio walioweka
Kiswahili katika matini kwa kutumia hati za Kiarabu (Kemima 2001). Hili ndilo
pengo la kitaaluma aliloligundua na analishughulikia kama ifutavyo.
Mwandishi
ameuanza mjadala wake kwa kufafanua maana ya uislamu. Anasema uislamu ni neno
lenye asili ya Kiarabu likiwa na maana ya amani, usafi na kujitolea, hivyo dini
ya kiislamu inaweza kutazamwa kama hali ya mtu au binadamu kujitoa mwenyewe na
kuyakubali mafundisho na misingi ya Allah. (mwenyezi Mungu).
Mwislamu
ni mtu yeyote anayekubali mafundisho na misingi ya Allah. Allah alitoa misingi
hii ya imani ya dini ya kiislamu kupitia kwa mtume wake mtukufu Muhammadi.
Misingi
ya imani hii ilitolewa kwa lugha ya Kiarabu ambayo mpaka sasa bado inatumika
kama lugha ya kutolea mafundisho ya imani ya dini ya kiislamu ijapokuwa lugha
nyingine zinatumika kutolea ufafanuzi wa maneno hayo .
Baadaye
mwandishi wa makala anatufahamisha kuhusu historia ya kuingia kwa dini ya
Kiislamu hapa Afrika Mashariki. Anahusisha suala hili na maingiliano ya kijamii
kati jamii za pwani ya Afrika Mashariki na
wageni kutoka Mashariki ya Kati na
Mashariki ya Mbali yaliyokuwapo karne nyingi zilizopita.
Kadhalika,
kuingia kwa dini ya Uislamu Afrika Mashariki na maeneo mengine kumehusishwa na
kipindi cha Hijira mwaka 622 AD.
Hijira kilikuwa ni kipindi cha mtawanyiko, ueneaji au uhamaji wa watu
kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kipindi hiki kilikuwa na ugomvi
baina ya waislamu na wasiokuwa waislamu na kusababisha adhabu na usumbufu
mkubwa.
Waarabu
wengi waliokuwa waislamu walihama kutoka
Mecca na kusambaa duniani kote. Watu walisumbuka maeneo ya kwenda kutokana na
imani ya dini yao, ndipo walipokimbilia Afrika hususani Misri, Ethiopia na
wengine walikuja Afrika Mashariki. Waarabu waislamu wa mwanzo kuja Afrika
Mashariki walikuwa ni pamoja na mfalme al Husain ibn Ali na watoto wake wa
kiume sita, walifikia maeneo ya Manda, Pate, Tanga, Mafia na Kilwa katika
Afrika Mashariki na maeneo ya Komoro.
Waarabu
walipofika Pwani ya Afrika Mashariki walianza kuingiliana na wenyeji wa upwa
huo (Waswahili). Maingiliano ya kiutamaduni baina ya makundi haya mawili
yalipelekea kuathiriana kiimani na vitu vingine vya kiutamaduni mfano, masuala
ya ndoa, mavazi, vyakula, urithi na uchukuaji wa leksimu katika lugha.
Waswahili
wengi walijiunga na dini hiyo ya kiislamu, na kwa njia hii Waswahili
wasingeweza kuepuka kujifunza lugha ya Kiarabu ili waweze kuielewa Kurani.
Pamoja
na hayo utamaduni wa Kiarabu ulikuwa na vitu vingi zaidi kuliko utamaduni wa
Waswahili na hii ilipelekea Waswahili wengi kuukubali utamaduni wa Kiarabu kwa
haraka. Matokeo yake utamaduni wa Waswahili uliiga mambo mengi kutoka katika
utamaduni wa Kiarabu, kama vile; katika leksimu maneno ya Kiarabu ni kama Allah, mola, subuhana, maulana, karama,
kurani, tawadha, ramadhani, swala, msikiti, kaaba, kibra, bismilahi.
Kiutamaduni
Waswahili walivutiwa na namna ya uvaaji kwa mfano wanawake kuvaa hijabu na ushungi na kwa upande wa wanaume huvaa magauni marefu yaitwayo kanzu. Pia sheria zao za ndoa
ziliongozwa na kanuni za dini ya kiislamu ziitwazo sharia.
Ujio
wa wageni ulivyozidi kuongezeka katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki
wageni hao walipokelewa na wenyeji Waswahili waliokuwa wamesilimu. Wageni hao
walipata makazi mapya kutoka kwa wenyeji waislamu, Waarabu waliingiliana na Waswahili
na hivyo kusababisha kuoana baina yao.
Walijifunza
utamaduni wa Waswahili na lugha ya Kiswahili wakati huohuo waliweza kubadilisha
imani za Waswahili na kuwaingiza katika uislamu. Makazi yao yalikuwa katika
maeneo ya Lamu, Mombasa, Zanzibar na maeneo mengine ya pwani ya Afrika
Mashariki.
Katika
makazi hayo walijishughulisha na biashara ambapo baadae zilikua na kufika
Afrika ya Kati, katika maendeleo yote hayo Waarabu hawakuitenga dini yao katika
maeneo yao ya kazi mfano huko Zanzibar Kiswahili chini ya Sultani Seyyid Said
wa Omani alipoanzisha makazi 1982 na kuhamia kabisa 1840 alikuta Kiswahili
kimekwisha enea na kuwa lingua franka.
Utawala
wa sultani huyo na watawala wengine chini yake walijifunza lugha hiyo na
kuifanya kuwa lugha ya kiutawala iliyopelekea Kiswahili kuwa na hadhi ya juu.
Katika
kuenea kwa dini hii Waarabu na Waswahili waliosilimika walijihusisha na
biashara na katika biashara zao walitumia lugha ya Kiswahili, hatimaye
kuiwezesha lugha hii kusambaa katika maeneo ya ndani au ya bara. Katika kila
kituo cha biashara waliweza kujenga misikiti ili wanapopata mapumziko yao
waweze kuswali. Vituo vya kibiashara vya
bara kutoka pwani kama vile Tanga, Bagamoyo, Tabora, Shinyanga, Kigoma
hadi Kongo ambako mfanyabiashara mwaarabu maarufu aliyekuwa mwislamu kwa asili
aliyeitwa Hemed Mohammed Er Murjeb akijulikana kwa jina la TIPU TIP alitumia
Kiswahili katika shughuli nzima ya biashara.
Watu
waliijua lugha ya Kiswahili kama lugha ya waungwana yaani watu waliostaarabika.
Katika vituo hivyo walijenga shule za kiislamu karibu na misikiti yao, madarasa yalijengwa kwa ajili
ya kuwafundishia wenyeji namna ya kusoma, kuandika na misingi ya dini ya
kiislamu. Lugha ya kufundishia ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa
upandse mwingine katika misikiti lugha ya Kisawhili na Kiarabu vilitumika kama
lugha ya mawasiliano. Kwa njia hii lugha ya Kiswahili ilionekana kukubalika
sana na wenyeji na kupelekea kusambaa bara na maeneo ya mbali, hivyo wakati
dini ya kiisalmu ikiendelea kusambaa na lugha ya Kiswahili ilizidi kusambaa kutokana
na lugha hiyo kueneza dini ya kiislamu.
Nchi
nyinginezo kama Rwanda lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda
kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19. Waislamu Waswahili
waliwasaidia Wajerumani kama wapagazi na wakalimani. Kwa kutumia fursa hii,
Waswahili na bila shaka waislamu walieneza dini yao kwa kutumia lugha ya
Kiswahili.
Lugha
ya Kiswahili pia ilitumika katika elimu kwa mfano katika kufundishia shule za
kijadi. Chifu wa Rwanda Yuhi Masinga alikubali kujifunza Kiswahili pamoja na
watawala wa Rwanda wa wakati huo ili kukuza mahusiano baina yao na Wajerumani.
Kipindi
hiki kinahusishwa sana na kuasisiwa kwa luha ya Kiswahili ncjini Rwanda
(Shabani1983).
Kwa
upande mwingine, Geraldi (1981) anasema kuwa Kiswahili kiliingia nchini Uganda
kabla ya mwaka 1862 kupitia biashara ya masafa marefu. Kama ilivyokuwa kwa
upande wa Rwanda, dini ya kiislamu ilichangia kuenea kwa lugha hii katika eneo
hili.
Anaeleza
kwamba Waswahili waliokuwa waislamu katika makampuni ya wafanyabiashara wa
Kiarabu walianzisha ligha hii nchini Uganda. Ilipokelewa na kuanza kutumika kwa
mara ya kwanza katika mahakama za kifalme.
Wazo
hili liliungwa mkono na Khatibu (1983:31) anasema Kabaka Mwanga alikuwa
mzungumzaji mzuri wa lugha ya Kiswahili akifanya mawasiliao na utawala wa
Kiingereza uliokuwa na makao yake Zanzibar hivyo Kiswahili kilienea sambamba na
uislamu katika ngome ya Buganda na hivi leo nchi ya Uganda ina kipao mbele
katika kusambaza Kiswahili mfano katika Chuo Kikuu cha Uislamu Uganda ni moja
ya mifano ya asasi kubwa zainazoshughulika na kufundisha, kufanya utafiti na
kutoa mafunzo mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili ingawa sera ya lugha nchini
Uganda haikukipa fursa Kiswahili kuenea zaidi.
Mwisho
nchini Burundi bwana Marcel (1983:55) anathibitisha kuwa Waarabu ndio
waliloeneza Kiswahili nchini humo ijapokuwa hakueleza mbinu walizotumia katika
kueneza Kiswahili hicho.
DATA ALIZOZITUMIA.
Alisoma vitabu na
makala mbalimbali. Vitabu na
makala hayo vmeorodheshwa mwishoni mwa makala haya. Kwa ufupi, makala yake
imetokana na data za utafiti wa maktabani.
HITIMISHO
Mwandishi
anahitimisha kwamba pamoja na mchango wa biashara, dini ya kikristo, utalii na
mambo mengineyo kuchangia katika maendeleo ya Kiswahili lakini uislamu hauwezi
kusahaulika, kutokana na jinsi kilivyochangia maendeleo ya Kiswahili Afrika ya
Mashariki na kati kwa ujumla.
MAMBO YA MSINGI
Mambo
ya msingi anayoelezea mwandishi ni pamoja na chimbuko la uislamu hapa Afrika
Mashariki: anasema kuwa uislamu uliletwa na Waarabu, ulikuja kabla ya dini ya
kikristo, ulichangia kwa kiasi kikubwa kukuza na kueneza Kiswahili kabla ya
mataifa ya Ulaya.
Uislamu
ulikuwa sambamba na shughuli za kibiashara, Waswahili waliokuwa wamesilimika
ndio waliohusika kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kueneza Kiswahili pwani ya
Afrika ya Mashariki na Bara hata kufika Afrika ya kati.
Anakubali
kwamba Kiswahili kinatumika kama lugha ya pili katika kufundishia dini ya
kiislamu Afrika ya Mashariki na Kati, wakati huohuo Kiswahili kilikuwa kama
lingua franka.
MCHANGO
WAKE KATIKA TENDI
Mwandishi
anakiri kuwa historia ya Waswahili ilikuwa katika masimulizi, hivyo ujio wa
Waarabu uliweza kuhifadhi fasihi hiyo
sumilizi katika matini kwa kutumia hati za kiarabu kwa mara ya kwanza na
wanazuoni wa Kiarabu. Hii ndiyo ilikuwa fasihi ya Waswahili iliyohifadhika
katika maandishi ikieleza dhamira za maadili ya jamii yao kwa mfano kufanya
kazi, umuhimu wa dini kwa watu, umuhimu wa familia ambapo ni miongoni mwa
dhamira nyingi ambazo zinajadiliwa katika tendi nyingi za Kiswahili mfano wa
tendi hizo zinazojadili dhamira hizi ni Utendi
wa Hamziyya, Tambuka, Herakali,
Inkishafi na Utenzi wa Mwana Kupona.
Baadhi
ya tendi hizi zinatupa mwelekeo kuwa zilikuwepo hata kabla ya biashara ya
utumwa, mfano utenzi wa Herakali
ambao hujulikana kama utendi wa Tambuka
wa mwaka 1728.
MAMBO
YALIYOELEZWA KINYUME NA UKWELI WA MAMBO
DHIMA YA WANALEKSIKOGRAFIA KATIKA
KUKUZA LUGHA YA KISWAHILI
Mwandishi anadai kuwa wazungu
walioeneza Kiswahili kipindi cha Uingereza walikuwa wanaleksikografia. Hii si
kweli kwani wao walikuwa wafanya biashara, wapelelezi na wamishionari tu. Lengo
la kuandika kamusi lilikuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia wazungu wenzao kujifunza
lugha kutoka huko kwao ili wakija pwani ya Afrika Mashariki waweze kuwasiliana
vyema na wenyeji, ili wapate malighafi kutoka Afrika Mashariki.
UTAMADUNI WA KIARABU UNA VITU VINGI VYA
KIUTAMADUNI KULIKO WA KISWAHILI
Mwandishi
anadai kuwa kuja kwa Waarabu pamoja na dini ya kiislamu kulichangia sana
maendeleo ya lugha ya Kiswahili kwa sababu utamaduni wa Kiarabu ulikuwa na vitu
vingi vya kiutamaduni.
Hoja hii haina mashiko kwa sababu
historia inaonyesha kuwa mahusiano ya kibiashara ndiyo yaliyopelekea kuwepo kwa
maingiliano ya kijamii na hatimaye kusababisha hali ya kuazimana na
kubadilishana mila na desturi miongoni mwa jamii zilizohusika. Kwa mfano kutoka
Asia, Waswahili walipata vitu kama vile nguo na shanga, kwa upande mwingine
jamii za Afrika Mashariki zilitoa bidhaa kama vile ngozi za wanyama, magamba ya
kobe, pembe za ndovu na nyinginezo. Bidhaa hizo zilipelekwa nchi za nje kama
vile India.
HOJA
NZITO: Dhima ya Dini ya Kiislamu
Dini
ya kiislamu imechangia kukuza na kueneza Kiswahili Afrika Mashariki na Kati.
Kadhalika imechangia katika kuathiri fasihi ya Kiswahili.
Mambo yaliyochangia au kuchochea athari
za Kiarabu katika isimu na fasihi ya Kiswahili toka Arabuni ni pamoja na elimu
ya madarasa kama vile kusoma na kuandika lugha ya Kiarabu, kusoma kaswida, sira
ya mtume.
Pia taaluma ya tafsiri ambapo hadithi
za mtume zilitafsiriwa kutoka lugha ya Kiarabu kwenda katika lugha ya
Kiswahili, pia tafsiri za Kuran. Mbali na elimu ya madrasa, kulikuwepo pia
elimu katika ngazi mbalimbali hadi mpaka katika ngazi ya chuo kikuu.
Maingiliano hayo yalichangia jamii hizi
kuazimana mila na tamaduni mbalimbali ikiwemo fasihi na isimu. Kwa mfano, kuingia kwa hati za
maandishi ya lugha ya Kiarabu kulichangia mambo kadhaa kama vile kuiweka na
kuihifadhi historia ya Waswahili katika maandishi kwa kutumia hati ya Kiarabu.
Ni wazi kuwa Afrika kulikuwa na tendi
ambazo zilikuwa katika masimulizi ambapo baada ya ujio wa Waarabu zikawekwa
katika maandishi, Mfano Hamziyya,nk
MAPENDEKEZO
Katika mjadala wake hajatuonyesha kuwa
uislamu unajitenga na biashara. Hivyo ni vema angezungumzia uislamu bila
kuambatanisha na biashara, kama walivyotueleza wakristo kuhusu dini yao. Kwa
maana hiyo angeweza kutueleza kuwa Kiswahili kimeenezwa na biashara na si dini.
Vinginevyo athibitishe kuwa dini ya Kiislamu imefungamana na kada nyinginezo za
maisha kama vile biashara, ndoa, na kila kitu katika maisha.
Kwa maana hiyo, tulitaraji pia
mwandishi aeleze utata wa mada zihususo dini na fasihi. Mtazamo wa dini ya
kiislamu na dini ya kikristo kuhusu sanaa, na maisha kwa jumla ni mmoja? Labda
hiki ndicho kilichowafanya wahakiki wa mwanzo kutojadili dhima ya dini ya
kiislamu katika kukuza lugha ya Kiswahili na fasihi ya Kiswahili.
HOJA TETE
Utafiti ufanyike ili kujua uwezekano wa
tendi hizi kama ziliwahusu Waswahili na utamaduni wao au ziliwahusu Waarabu
kwani maudhui ya tendi nyingi kati ya hizi alizorojelea mwandishi yanaelekea
kujadili maadili na maonyo ya jamii ambazo zinahusiana sana na uislamu.
MAREJEO
Bosha, I. (1993). Taathira
za Kiarabu Katika Kiswahili Pamoja na Kamusi Thulathiya. Dar es Salaam: Dar
es Salaam University Press
Bosha, I.1994. Athari
za Kiarabu katika Kiswahili Sanifu. Tasnifu ya Uzamili (Isiyochapishwa), Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
Chimerah, R.1998. Kiswahili:
Past, Present and Future Horizons. Nairobi: Nairobi University Press
Chiraghdin, S. na
Mnyampala, M. 1977. Historia ya Kiswahili. Nairobi: O.U.P.
Gerard, Albert 1981. African
Language Literatures: An Introduction to the Literary History of Sub- Saharan
Africa. Harlow: Longman Burntmill (pp. 93 – 153)
Kimemia, J. N. 2001. Kiswahili:
The Dilemma of Developing The National Language. Egerton University Press
Khatib, M. S. 1983.
Historia na Maendeleo ya Kiswahili Zanzibar. Katika: TUKI. Lugha ya
Kiswahili. Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili 1. Dar
es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (uk. 19 – 50)
Marcel, B.1983. Lugha
ya Kiswahili Nchini Burundi. Katika: TUKI. Lugha ya Kiswahili. Makala za
Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili I. Dar es Salaam: Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (uk. 55 – 61)
Massamba, D. P. B.
1986. “On the Inflence of Local Languages on Kiswahili: The case of Mara Region
in Tanzania.” In: Kiswahili: Juzuu 53/1 na 53/2 (pp. 67 – 83)
Mazrui, A.A. and A.
Mazrui, 1995. Swahili State and Society: The Political Economy of an African
Language. Nairobi: East African Education Publishers
Mbaabu, I. 1978. Kiswahili
Lugha ya Taifa. Nairobi: K.L.B
Mbaabu, I. 1985. New
Horizons in Kiswahili. Nairobi: K.L.B
Mbaabu, I. 1991. Historia
ya Usanifishaji wa Kiswahili. Nairobi: Longman Kenya Ltd. The Journal of
Pan African Studies, vol.2, no.8, March 2009
Mukuthuria, M. 2001.
Matatizo Yanayokabili Kiswahili Karne ya Ishirini na Moja. Katika: Islamic
University Journal, Vol. 2 No.2, Mbale – Uganda (uk. 135 – 142).
Mwongera, N.S. 1994.
An Economic History of the Imenti of Mt. Kenya, 1800 – 1945.
[Unpublished M. Phil. Thesis] Moi University.
Nurse, D. and Spear,
T. (1985) The Swahili: Reconstructing the History and Language of an African
Society, 800 – 1500. University of Pennsylvania Press.
Ogutu, M. A. and
Kenyanchui, S. (1987) An Introduction to African History up to 1885.
Nairobi: College of Adult and Distance Education, University of Nairobi.
Prins, A.H.J. (1967) Swahili
Speaking Peoples of Zanzibar and the East African Coast. London:
International African Institute.
Sengo, T. S. Y. (1998)
Kiswahili na Uisilamu Afrika Mashariki. Unpublished Semina Paper, Islamic
University in Uganda.
No comments:
Post a Comment