Hatimae mahakama
nchini Misri imemhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani, mwanaharakati maarufu
Alaa Abdel Fattah, aliyetoa mchango mkubwa katika harakati za kuuangusha
utawala wa rais Hosni Mubarak mwaka 2011, kwa makosa ya kumshambulia askari
polisi wakati wa maandamano haramu.
Alaa ambaye
alikuwa nje kwa dhamana tangu mwezi Machi, amekamatwa mara moja na washtakiwa
wengine wawili baada ya kutolewa hukumu hiyo wakati wakisuburi kuruhusiwa
kuingia katika mahakama hiyo ya muda iliyoundwa kwenye chuo cha polisi mjini
Cairo.
Mahakama hiyo
imetoa hukumu sawa na hizo kwa washtakiwa wengine 24, ambao wote hawakuwa
mahakamani, baada ya kuwatia hatia kwa makosa yanayoanzia kwenye kushiriki
maandamano yanayokiuka sheria hadi kwenye kufanya vurugu, kufunga barabara na
kuwashambulia maafisa wa polisi.
Hatua hio imekuja,
ikiwa ni siku chache tu ambapo mahakama nchini humo iliwahukumu raia kadhaa
adhabu ya kifo kwa tuhma za kukutikana na makosa ya uvunjifu wa amani na kusababisha
watu wawili kupoteza maisha yao.
No comments:
Post a Comment