Hali ya
taharuki imezidi kutanda mjini Mombasa nchini Kenya kufuatia kupigwa risasi na
kuuawa Sheikh Muhammad Idriss aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na
Wahubiri wa Kiislamu CIPK.
Kamishna
wa polisi mjini Mombasa Nelson Marwa amesema kuwa, polisi wamejipanga na wamewekwa
katika maeneo mbali mbali ili kuhakikisha usalama kwa raia unalindwa.
Sheikh
Idriss aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake saa kumi na moja alfajiri
ya kuamkia Jumanne wakati alipokuwa anaelekea katika Msikiti wa Swalihina
ulioko takribani mita 50 tu kutoka nyumbani kwake.
Kwa muda
mrefu Sheikh Idriss alikuwa mwenyekiti na Imamu wa Msikiti wa Sakina mjini
Mombasa kabla ya kuondolewa kwa lazima na vijana wanaodaiwa kuwa wenye itikadi
kali kwa kile kinachodaiwa kuwa sheikh huyo alikuwa mnafiki.
No comments:
Post a Comment