Watu wasiojulikana leo asubuhi wamempiga risasi na kumuua Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kiislamu Keny
a Sheikh Mohammad Idris huko Likoni mjini Mombasa.
Sheikh Idris amepigwa risasi nje ya nyumba yake saa kumi na moja
alfajiri wakati alipokuwa anaelekea katika Msikiti wa Swalihina ulioko
takribani mita 50 kutoka nyumbani kwake.
Kwa muda mrefu Sheikh Idris alikuwa mwenyekiti na Imamu wa Msikiti
wa Sakina mjini Mombasa kabla ya kuondolewa kwa lazima msikitini hapo.
Mwanazuoni huyo mwandamizi wa Kiislamu mjini Mombasa hivi karibuni
alisema kuwa ana wasiwasi na usalama wa maisha yake baada ya baadhi ya vijana kutisha kumuua.
Miezi kadhaa iliyopita Sheikh Idris alisema vijana wenye misimamo
mikali na ufahamu potofu kuhusu jihadi walikuwa wanakusanyika wakiwa na nia
mbaya dhidi ya nchi ya Kenya.
Aliwahi kutoa wito kwa polisi kukabiliana vilivyo na vijana hao
ambao alidai walikuwa wanazusha fujo kwa jina la Uislamu huko Mombasa.
Matamshi yake hayo yaliwakasirisha vijana hao ambao walidai kuwa sheikh
huyo eti ni msaliti.
Daima Sheikh Idris alikuwa akisisitiza kuwa Uislamu ni dini ya
amani inayopinga vitendo vya ugaidi.
Mwanazuoni huyo wa Kiislamu amezikwa leo alasiri mjini Mombasa.
Nae, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amelaani vikali mauaji hayo na
kusema serikali itahakikisha waliohusika wanatiwa mbaroni.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Kenyatta amesema,
‘Sheikh Idris alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya vijana wenye itikadi
kali na kifo chake ni pigo katika juhudi za kukabiliana na misimamo mikali ya
kidini nchini Kenya.
Kenyatta amemtaja marehemu Sheikh Idris kuwa mwanazuoni aliyekuwa
mnyenyekevu, mpenda amani, mwenye fikra huru na aliyejitolea maisha yake
kuwahudumia Waislamu kwa msingi wa Qur’ani Tukufu.
Naye kiongozi wa waliowengi katika Bunge la Kenya Adan Duale
amelaani mauaji hayo na kusema lazima waliohusika wafikishwe katika vyombo vya
sheria.
No comments:
Post a Comment