Polisi
nchini Afrika Kusini wanachunguza tukio ambapo mwanamume mmoja anaripotiwa
kumuaa mwaname mwingine aliyekuwa na uhusiano na kimapenzi na mwanamuke
anayeaminika kuwa mpenzi wake wa zamani.
Taarifa
zinasema kuwa mwanamme huyo alimuua na kumkatakata vipande na kisha kuula Moyo
wake.
Majirani
katika eneo la Malunga lililo katika mji wa Gugulethu nje ya mji wa Capetown,
wamesema kuwa walikumbana na mwanamume aliyeshuhudia mauaji hayo siku ya
Jumanne.
Mashuhuda
wamesema kuwa wakati walipofika katika mtaa wa kifaharai ambako mshukiwa
alikuwa anaishi walimsikia akisema kuwa "ni yeye mfalme" akisema kuwa
bado anampenda mpenzi wake wa zamani.
Vyanzo
vya habari vinaeleza kuwa Polisi walipofika eneo la tukio walimpata mshukiwa
akila moyo wa binadamu akitumia uma na kisu.
Aidha,
Polisi imefahamishwa kuwa mwathiriwa alidungwa kisu upande wake wa kushoto
kifuani na kwenye shingo yake na katika sehemu ya uso alikuwa na alama ya
kuumwa.
Marehemu
anayeaminika kuwa Bwana Mbuyiselo Manona,alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke aliyekuwa mpenzi wa mshukiwa kwa miaka minne.
Hata
hivyo, imedaiwa kuwa hapakuwa na dalili zozote za mwanamke huyo nyumbani kwake
Jumatano lakini gari lake lilikuwa limeegeshwa nyumbani kwake.
Inaripotiwa
kuwa si mara ya kwanza mwanamke huyo ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka
50 kuhusishwa na visa vinavyohusiana na mapenzi.
No comments:
Post a Comment