Mlipuko unaosadikiwa kuwa ni bomu umelipuka katika
eneo la Darajani Zanzibar na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi
watatu.
Tarifa zinasema kuwa mlipuko huo umetokea baada ya waumini wa dini ya kiislamu kumaliza
muhadhara uliokuwa ukitolewa Miskiti hapo baada ya salsa ya Ishaa.
Hayo yanajiri
huku matokeo ya milipuko yakiendelea kuripotiwa mara kwa mara ndani na nje ya
Zanzibar, huku ikiaminika kuwa kunawatu wenye nia ya dhati ya kutaka kuichafua mandhari
ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi
imebeba sifa ya kuwa ni kisiwa cha amani, upendo na ukarimu.
Wakazi wa darajani wamesema kuwa baada ya
kumalizika kwa muhadhara huo ndipo waliposikia sauti ya mripuko na kusababisha
sintofahamu katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment