Dunia imezidi kuonekana kuwa mzimu wa shetani, baada ya kuacha
mafundisho sahihi ya Allah (SW) na kujikubalisha kuwa watumishi wa shetani kwa
kukana maumbile mazuri ambayo Allah (SW) amewaumba wanadamu na kutafuta njia
nyingine wanazozijua wao.
Hali hii inathibitishwa na kitendo cha Mtoto wa kike wa mfalme wa
R&B Robert Kelly aka R.Kelly mwenye umri wa miaka 14 ambaye amejitokeza
hadharani na kujitangaza kuwa amebadilisha jinsia na kuwa mvulana.
Mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Jaya ameitangazia dunia
kupitia mitandao ya jikamii huku akijigamba na kudai kuwa yeye sasa ni mvulana
na si msichana kama maumbile aliyopewa na Mwenyezi Mungu.
Awali dada huyo, aliyezaliwa na jinsia ya kike lakini ameonekana
kutokuridhia maamuzi ya Alla (SW) na kutafuta njia za kujibadilisha maumbile na
sasa anasema ni mvulana na jina lake jipya ni Jay.
Aidha, amesema kuwa pamoja na mama yake mzazi aitwaye Andrea Kelly kuonekana
kukubaliana na uamuzi aliouchukua, baba yake R.Kelly bado bado hajasema ch
ochote juu ya kidendo hicho.
Jay amesema alijigundua kuanza kuvutiwa na wasichana akiwa na miaka
6, lakini ameongeza kuwa bado hahitaji kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa sasa.
Dunia tunayoishi nayo sasa ni dunia ya ajabu kiasi kwamba wanadamu
wakotayari tu kukana chochote kile kinachotokana na utukufu wa Allah (SW) bila
kujali mustakbali wa baadae.
Ikumbukwe kuwa ni hivi karibuni tu baadhi ya viongozi wa juu wa
kimataifa wamekuwa wakiutangazia ulimwengu juu ya kufaa kwa matendo ya kishenzi
ya ushoga.
Aidha, viongozi hao ndio wamekuwa msitari wa mbele kuyalazimisha
mataifa machanga kuukubali unyama huo kwa nguvu.
No comments:
Post a Comment