Sunday, June 1, 2014

BANKOK Maelfu ya polisi pamoja na wanajeshi wamepelekwa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok kwa jaribio la kuangamiza maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi jana. Baadhi ya vituo vya treni pamoja na maduka ya jumla yamefungwa kutokana na maandamano hayo. Mashuhuda mjini Bangkok wamesema kuwa eneo la biashara katikati ya mji huo limesalia kuwa mahame baada ya jeshi kulifunga. Siku ya ijumaa kiongozi wa jeshi Jenerali Prayuth Chan Ocha aliziambia pande pinzani kushirikiana na kuwacha maandamano ili kuleta maridhiano. Katika hotuba hiyo kiongozi huyo amesema kuwa uchaguzi mpya hautaitishwa hadi baada ya mwaka mmoja.

1 comment:

  1. Maelfu ya polisi pamoja na wanajeshi wamepelekwa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok kwa jaribio la kuangamiza maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi jana

    ReplyDelete