Sunday, June 1, 2014

ZANZIBAR. Majaji mjini Zanzibar wameendelea kuilalamikia serikali kutokana na kuondolewa kwa ulinzi wa jeshi la polisi nyumbani kwao jambo wanalodai linahatarisha uhai wa maisha yao. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu amethibitisha kuwapo kwa hali na kusema kuwa mamlaka husika imeanza kufuatilia. Aidha, Jaji Makungu amesema awali waliwahi kujadili juu ya suala hilo na kufikia hatua nzuri ambapo, vikosi maalumu vya SMZ ndiyo vingepaswa kufanya kazi hiyo. Naye, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame amesema ni kweli kwamba askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia(FFU) ambao walikuwa wakihusika na shughuli hizo wameshaondolewa kwenye shughuli za ulinzi Hata hivyo, amesema tayari wameshapeleka mapendekezo yao kutaka kila nyumba ya jaji kujengwa kibanda maalumu kwa ajili ya walinzi, lakini jambo hilo halijafanyiwa kazi hadi sasa.

No comments:

Post a Comment