Watu zaidi ya 100 wamefariki dunia na mamia ya
wengine wamebaki bila ya makaazi kutokana na mafuriko yaliyoukumba mkoa wa
Baghlan nchini Afghanistan.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, mafuriko
hayo yameyotokea usiku wa kuamkia jana huku yakisomba na kuharibu mamia ya
nyumba.
Ripoti zinaeleza kuwa waathirika wa janga hilo
ni wakaazi wa wilaya ya Gozar Gahe, huku ikihofiwa kuwepo uwezekano wa
kuongezeka idadi ya vifo, kutokana na baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa idadi ya
watu waliofariki ni 200.
Mnamo mwezi Aprili zaidi ya watu 150 walifariki
na maelfu ya wengine kubaki bila ya makaazi baada ya mafuriko kuikumba mikoa ya
Faryab, Sar-e-Pol, Jowzan na Badghis nchini Afghanistan.
Majanga kama hayo ya kimaumbile husababisha
maafa makubwa ya roho za watu na mali kutokana na nyumba nyingi nchini humo
kujengwa kwa kutumia udongo wa tope na mawe hali inayosababisha kusombwa
kirahisi na maji.
No comments:
Post a Comment